Ni muda sasa takribani miaka mitatu kikosi cha Simba SC kimekuwa hakina muendelezo mzuri wa kimatokeo jambo ambalo limepelekea kushindwa kuchukua mataji makubwa nchini.

Mashabiki na wapenzi wa Soka nchini waliishuhudia Simba SC bora miaka minne iliyopita ikiwa imeimarika kila idara kuanzia golini, beki, Kiungo na ushambuliaji na hata ubora wa wachezaji wake kikosini wanaoanza na wanaotokea “Sub” jambo ambalo hata akikosekana mchezaji mmoja ilikuwa hakuna tatizo lolote timu inacheza soka safi na matokeo yanapatikana.

Mabadiliko na timu kuanza kutofanya vizuri ikaanza kudhihirisha kushuka kwa ubora wa timu hiyo na dhahiri shahiri mapungufu yakaanza kuonekana, sasa maeneo yapi ambayo Kocha mkuu wa sasa Fadlu Davids anapaswa kuyafanyia maboresho makubwa kikosini na timu kwa ujumla kuwa na muunganiko mzuri kimfumo na kimbinu ili kuweza kufaulu mtihani huu mzito kwake.

Moja, eneo la ulinzi, moja ya eneo ambalo lilikuwa na changamoto kubwa msimu uliyopita ni eneo lao la ulinzi kulikuwa na mapungufu kadhaa hususa beki wa kati kulikuwa na kutoelewana kwa mabeki wa kati jambo ambalo lilipelekea makosa binafsi ya Mara kwa mara, na kitakwimu waliruhusu magoli…… katika michezo 30 ya Ligi kuu ya NBC, Fadlu pamoja na benchi lake la Ufundi wanapaswa kulifanyia kazi eneo ilo kwani eneo la beki ndiyo eneo mama linaloweza kukulindia matokeo na kushinda mechi.

Pili, eneo la kiungo, kutokuwa na kiungo imara cha ukabaji kilipelekea kuipa kazi kubwa sana eneo la beki, ilikuwa ni rahisi sana kuifikia beki pale timu inapofanyiwa shambulizi la haraka na la kushtukiza, matarajio makubwa ya wengi ni kuona maboresho makubwa yakifanyika kwenye eneo la kiungo mkabaji zaidi tatizo ambalo limedumu muda mrefu kwa kukosa kiungo asili mkabaji.

Pia muunganiko mzuri wa eneo la kiungo mshambuliaji, uimara wa kiungo cha ushambuliaji unatengenezwa kwa kuwa na kiungo mkabaji mzuri ambaye atakuwa na uwezo wa kuilinda “back four” yake pamoja na kuwa kiunganishi na kiungo cha ushambuliaji kutuliza mchezo, kiungo ambaye Simba SC walimkosa kwa muda sasa.

Eneo la mwisho ni ushambuliaji eneo ambalo linakupa sababu ya kupata ushindi na ilo ni moja ya eneo ambalo liliwatesa sana Simba SC msimu uliyopita hususa kwenye mzunguko wa pili kwa kukosa “Target man” ambaye ana uwezo kwa kutumia nafasi chache kwa usahihi.

Huo mtihani wa Fadlu Davids na kuna ishara kuwa ukifanikiwa kwa haraka basi itakuwa rahisi kwake na mapokezi mazuri ila ikichelewa itahitajika uvumilivu na imani kwa viongozi wa klabu hiyo.

SOMA ZAIDI: Simba Ni Daraja La Makocha Kupata Umaarufu?

2 Comments

  1. Pingback: Baada Ya Usajili Tuitegmee Yanga Ya Namna Gani Msimu Huu?

Leave A Reply


Exit mobile version