MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Stan Collymore amemtaka fowadi wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ajiunge na vilabu vya Premier League, Newcastle United au Aston Villa na kutofuata njia ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Collymore alisema hayo alipokuwa akimshauri Zaha dhidi ya kujiunga na klabu moja nchini Saudi Arabia, na kuongeza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anapaswa kuwaachia Ronaldo na Messi.

Ronaldo kwa sasa anachezea klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia na Messi, ambaye mkataba wake na Paris Saint-Germain utamalizika mwishoni mwa msimu huu, pia amekuwa akihusishwa na kuhamia Mashariki ya Kati.

Mkataba wa Zaha na Crystal Palace utamalizika msimu wa joto na bado hajaongeza mpaka sasa.

Raia huyo wa Ivory Coast amekuwa akihusishwa na kuhamia Mashariki ya Kati katika majira ya joto.

“Wilfried Zaha angekuwa kichaa kwenda Saudi Arabia. Tunajua kwamba pesa ni muhimu kwa wachezaji, lakini pia atashinda pesa nyingi huko London. Kuna vilabu vingi ambavyo bado vinaweza kusaidiwa na talanta yake huko England kama Newcastle au Aston Villa,” Collymore alisema (kupitia chapisho la Ufaransa Onze Mondial).

“Anapaswa kupuuza chaguo rahisi na kuwaachia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao tayari wamepata mafanikio makubwa zaidi.”

Leave A Reply


Exit mobile version