Moja kati ya mechi kubwa kwa siku ya leo hatua ya 16 bora katika michuano ya AFCON ni kati ya mabingwa mara nyingi wa michuano hii Misri (Egypt) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) mechi itakayoamua nani anatinga hatua ya robo fainali katika michuano hii kwa mwaka huu inayofanyikia nchini Ivory Coast.

Imekua AFCON ambayo bila shaka kumekua na matokeo ambayo sio ya kutegemea zaidi sana yamekua ya kushangaza lakini pia na matukio ambayo hayajategemewa kutokea fikiria kuhusu Misri ikiwa inacheza huku ikiwa inamkosa Mo Salah ambaye aliumia katika mechi ya 2 pekee katika michuano hii.

Katika michuano hii Egypt hawajashinda mchezo hata mmoja wala kufungwa zaidi ya kupata sare 3 pekee zilizowafanya waingie katika hatua ya 16 bora lakini pia namna ambavyo wameendelea kuwa na ubora kwa wachezaji kwani wamefunga takribani mabao 5 kati ya 6 katika michuano hii.

Kama ilivyo kwa mafarao ni hivyohivyo pia kwa DR Congo ambao hawajashinda mchezo hata mmoja wakipata sare michezo yao yote mitatu ambao ni dhidi ya Morocco, Zambia na Tanzania kwahiyo bila shaka wanataka kupambania kuona wanapata ushindi wa kwanza katika michuano ya msimu huu.

TUNASUKAJE MKEKA WA EGYPT vs DR CONGO?

Egypt wamekua wababe mbele ya DR Congo kwani wamewafunga takribani mechi 3 ambazo wamekutana zikiwemo za kufuzu kombe la dunia na zile za AFCON. Kutokana na mchezo huu ulivyo na jinsi AFCON ilivyokua na matokeo ya kushangaza katika mchezo huu tunaweza kutumia Masoko haya ya ubashiri:

Kubashiri katika magoli

Katika mchezo huu kwa upande wa magoli itakua moja kati ya njia nzuri ya kubashiri kwa masoko ya Over na Under. Kwanza kabisa kwa upande wa Egypt wamekua na rekodi ya kufunga katika kila mchezo kwenye michuano hii ya AFCON hivyo unaweza kumpa Egypt apate angalau goli 1 (Egypt Goals Over 0.5) lakini kutokana na jinsi ambavyo DR Congo katika michuano hii wameshindwa kupata walau mabao 3 basi unaweza kuweka DR Congo asifunge mabao zaidi ya 3 katika mchezo huu ( DR Congo Goals Under 2.5).

Kwa wale ambao wanapenda kubashiri upande wa kadi wanaweza kuweka mchezo mzima kupatikane kadi zaidi ya 5 yaani (Total Bookings Over 5) na hii iwe kwa timu zote.

Ukitazama kwa upande wa Player Specials pia tunaweza bashiri kuwa mchezaji wa Egypt Mostafa Mohamed apige walau shots on target 3 yaani Player Specials Mostafa Mohamed Total Shots Over 2.5 na hii ni kwa sababu katika michezo mitatu ya hatua ya makundi ameshinda goli katika michezo yote  huku kwa upande wa DR Congo unaweza kumpa apige walau mashuti 2 langoni yaani Silas Total Shots Over 1.5 na ni kwa sababu ni moja kati ya wachezaji hatari ambao wamekua wakiipambania vyema DR Congo katika michuano ya msimu huu.

SOMA ZAIDI: Nini Maana ya GG katika betting? 

 

Leave A Reply


Exit mobile version