Edwin Balua amejiunga Simba kutoka Tanzania Prisons, huu ni usajili wa mchezaji wa kizawa ambaye anakuwa wa tatu baada ya Karabaka na Chasambu. Usajili huu unakuja baada ya Simba kutoka kuachana na wachezaji wanne wazawa, swali la msingi hapa ni wapi wanafeli wachezaji wazawa hasa wakijiunga na klabu za Simba na Yanga.

Balua ni mchezaji mzuri ambaye ameonyesha kiwango ambacho kimewashawishi Simba kumsajili lakini ataweza kuendeleza kiwango chake ndani ya Simba? Eneo analocheza ni Winga wa kushoto au kulia,eneo ambalo limetawaliwa na wachezaji wa kigeni ambao wanafanya vizuri, maana yake ana kazi ya kumshawishi Benchikha ili apenye kwenye kikosi cha kwanza.

Tatizo ambalo wachezaji wengi wazawa wameshindwa kwenye klabu hizi za Simba na Yanga, sijui ni presha au wanaridhika wakifika kwenye hizi klabu. Lakini kitu cha msingi kwa Balua ni kuendelea pale alipoishia kwa sababu mpira ni mchezo wa wazi ukiweza kumshawishi mwalimu bila shaka utapata nafasi.

Tumeona kwa Dickson Job pale Yanga, Feisal Salum mbele ya wachezaji wa kigeni kwahiyo Edwin Balua, Ladack Chasambi na Karabaka wana uwanja mkubwa wa kujifunza kwanza kabla hawajaanza kupambania nafasi. Angalizo wasijekuwa kama Nassoro Kapama, Shaban Chilunda, Jimmyson Mwinuke na wengine.

Huwa kama taifa tunategemea makubwa kutoka kwa wachezaji ambao wanatoka timu za Daraja la kati na kuingia katika hizi timu kubwa lakini wapo amabo huweza kufanya makubwa lakini wapo ambao hushindwa kufikia matarajio ya wengi.

Kwa namna Fulani klabu ya Simba huchukua baadhi ya wachezaji wakiwa na viwango bora sana lakini hushindwa kutoboa na hatimaye kuporomoka viwango vyao.Kwa jinsi Simba wanavyo hitaji kurudisha utawala wao kwenye soka wanahitaji mtu wa kuja kufanya kazi na sio anae pigania kufufua kipaji chake au kukua kisoka.

Unadhani Usajili huu una tija kwa klabu ya Simba?

Endelea kusoma zaidi kuhusu makala mbalimbali kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version