Ile siku ambayo bila shaka kabisa mashabiki wa soka barani Afrika walikua wakiisubiria kwa hamu imewadia na kubwa ni kuhusu upangaji wat imu zitakazokutana hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Pamoja na lile la ligi ya mabingwa barani Afrika.

Hii inazihusisha timu 8 ambazo zimefuzu hatua ya robo fainali katika mashindano yote mawili yani shirikisho Pamoja na ligi ya mabingwa baada ya kufanya vyema katika hatua ya makundi na sasa ni hatua ya mtoano.

Nikukumbushe tu kuwa katika michuano hii nchi ya Tanzania pekee ndiyo ambayo imetoa timu 2 ambazo zimefuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika na timu ambazo zimefuzu ni Al Ahly (Egypt), ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire), Mamelodi Sundowns (South Africa), Atletico Petroleos (Angola), TP Mazembe (DR Congo), Simba SC (Tanzania), Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) na Young Africans (Tanzania).

Jinsi Droo Itakavyochezeshwa:

Kutakua na vyungu ambavyo vitatumika kuchezesha droo hii na itakua kama ifuatavyo:

Pot 1: Timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao

Pot 2: Kutakua na mipira midogo 3 ambayo itahusisha timu 3 lakini zilizokua nafasi ya 1 zilizokua Group A

Pot 3: Kutakua na mipira 3 midogo ambayo itahusisha timu 3 lakini kutoka nafasi ya 1 ya Group B.

Pot 4: Kutakua na mipira midogo 3 ambayo itahusisha timu 3 lakini zilizokua nafasi ya 1 zilizokua Group C

Pot 5: Kutakua na mipira midogo 3 ambayo itahusisha timu 3 lakini zilizokua nafasi ya 1 zilizokua Group D

Pot 6 – Litakua tupu.

Droo Itakavyochezeshwa

  • Utachukuliwa mpira mmoja kutoka Pot 1 ambao utaoneswa timu iliyochukuliwa
  • Utachukuliwa mpira kutoka Pots nyingine yaani (2, 3, 4 & 5) kasoro tu timu ambazo zilikua kundi moja ndio ambazo hazitachukuliwa Pamoja na itakayopatikana basi atacheza na yule aliyeoneshwa mwanzo.
  • Mipira 3 ambayo itachukuliwa basi itawekwa katika chungu tupu cha 6.
  • Itachanganywa mipira 3 katika Pot ili kuchagua nani anakutana na nani katika wale waliingia robo fainali kama timu ya 2.

Kutokana na sheria za mashindano ni wazi kuwa timu zote zilizoingia kama wa pili katika makundi yake basi watacheza michezo yao ya kwanza nyumbani na kumalizia ugenini.

SOMA ZAIDI: Hizi Ndio Pesa Za CAF Kwa Kila Hatua Ligi Ya Mabingwa

1 Comment

  1. Pingback: Ratiba Kamili Ya Robo Fainali Ligi Ya Mabingwa Afrika - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version