Ukiachilia mbali mchezo kati ya Nigeria na Angola mchezo mwingine wa pili wa kombe la mataifa barani Afrika hii leo hatua ya robo fainali ni kati ya DR Congo dhidi ya Guinea mchezo ambao utatoa timu itakayoenda kucheza nusu fainali dhidi ya Mali au Ivory Coast.

TAKWIMU:

DR Congo wamefuzu hatua hii kwa kumfunga Misri katika hatua ya 16 bora kwa njia ya penati 8 kwa 7 mechi ambayo mpaka dakika 120 iliisha kwa bao 1:1 mpaka kufika hatua ya matuta wakati Guinea wamefuzu kwa kuwafunga Equatorial Guinea bao 1:0 ambao walipungua na kuwa 10 baada ya kupata kadi nyekundu dakika ya 53.

Kumbuka kuwa hii ndio mara ya kwanza kwa Guinea kushinda katika hatua ya mtoano na kufuzu hatua inayofuata wakati  DR Congo wao mara ya mwisho kuingia hatua ya robo fainali ni mwaka 2017.

  • Hii ni mara ya 8 wanakutana kati ya DR Congo vs Guinea ambapo mpaka sasa Congo anaongoza kwa kumfunga Guinea mara 4 huku Guinea akishinda mara 2 pekee na sare 2.
  • Mechi 6 za mwisho za Guinea zimekua na magoli chini ya matatu.
  • Katika michuano hii ni goli moja pekee limefungwa katika kipindi cha kwanza katika mechi zinazowakutanisha Guinea ambapo ni mechi 4 katika 3 za makundi na 1 ya 16 bora.
  • Congo wamepata sare katika michezo yao yote msimu huu.

TUNABETIJE?

DR Congo bila shaka watataka kuumaliza mchezo huu mapema ili wafuzu nusu fainali lakini msimu huu michuano ya mataifa barani Afrika imekua na matokeo ya kushangaza kabisa n ani wazi utakua mchezo mgumu.

  1. Kutakua na kufungana vipindi vyote – NO (Both Halves GG-NO)
  2. Kutakua na magoli zaidi ya 1 (Over 1.5)
  3. Kutakua na kona zaidi ya 5 (Over 4.5 Total Corners)

SOMA ZAIDI: Nigeria vs Angola Tunasuka Hivi Mkeka

1 Comment

  1. Just wanted to let you know how impressive I find your article to be. The clarity of your post is remarkable, leading me to believe that you are an authority on this subject. If it’s okay with you, I’d like to subscribe to your feed in order to be notified of future posts. Your work is truly appreciated. Please continue this gratifying endeavor.

Leave A Reply


Exit mobile version