Unaweza kusema ni moja kati ya mchezo ambao bila shaka mashabiki wa soka walikua makini sana kuutazama na kila mmoja alikua anatamani kuona nani atapata ushindi wa kwanza katika michuano hii ikumbukwe kuwa katika hatua ya makundi wote wawili yaani DR Congo Pamoja na Egypt hakuna ambae alishinda mchezo hata mmoja zaidi ya kupata sare ambazo zimewapeleka mpaka hatua hii ya 16 bora.

Katika mchezo ambao umewakutanisha mabingwa hawa wa zamani wa michuano hii ya mataifa barani Afrika tumeona namna ambavyo kumekua na matokeo ambayo yamekua hayatarajiwi na wengi kutokana na namna ambavyo timu zilivyokuja katika michuano hii zikiwa zimefanya uwekezaji mkubwa na maandalizi mazuri zaidi kwa ajili ya michuano hii.

DR Congo aliingia kama timu dhaifu mbele ya Egypt na hii ni kwa sababu ameshapokea vipigo kadhaa kutoka kwa Egypt kuanzia zile mechi za kufuzu kombe la dunia mpaka baadhi ya mechi za mataifa ya soka barani Afrika.

Mchezo huu mpaka kwenda hatua ya maamuzi ya penati ilikua ni bahati tu kwa timu ya taifa ya Egypt kwani sio timu ile ambayo ilikua sumbufu sana kama ambavyo ilikua miaka iliyopita lakini pia tuwapongeze DR Congo namna ambavyo walikuja na mikakati mizuri ya kuwaheshimu mabingwa hawa wa kihistoria wa michuano hii.

Nilitegemea sana jambo hili kwasababu ukikitazama kikosi cha Misri ni kama hawakua tayari na michuano hii kuanzia kwa namna ambavyo wamekua wakiruhusu magoli ya kizembe kabisa ambazo ni wazi kabisa lawama zinaanzia kwa mabeki wao lakini pia jambo kubwa zaidi majeruhi kwa wachezaji wao muhimu kabisa ni jambo ambalo limewaangusha kabisa katika michuano hii.

SOMA ZAIDI: Namibia Imetuonesha Umuhimu Wa Kumuamini Kocha Mzawa

 

1 Comment

  1. Pingback: Waliotegemewa Wameduwazwa Na Wasiotegemewa AFCON - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version