Ni zaidi ya misimu kumi sasa vilabu hivi vinashiriki Ligi kuu ya Tanzania kwa nyakati tofauti tofauti huku ikiitwa majina ya wadhamini mbalimbali, vilabu hivyo vimekutana mfululizo kila msimu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tokea ikiitwa Vodacom Premier League maarufu kama VPL, ikaaitwa tena Tanzania Premier League (TPL) na sasa inaitwa NBC Premier League bado wanaendelea kukutana.

Wanaozungumziwa hapo ni vilabu viwili ambavyo vinakutana kwenye mchezo wa pili wa raundi ya pili, mchezo wa Ligi kuu ya NBC 2023/2024 ambavyo ni Simba SC na Tanzania Prisons huku mchezo wa kwanza msimu huu walipokutana Simba SC alishinda 3-1 kwa magoli ya Clatous Chama, John Bocco na Saidi Ntibazonkiza kwa upande wa Simba SC huku Edwin Balua akiwafungia Tanzania Prisons.

Kitakwimu mpaka sasa vilabu hivi vimekutana mara Saba kuanzia msimu wa 2020/2021 hadi msimu huu, ambapo Simba SC amekuwa akimuonea Tanzania Prisons kwa kushinda michezo minne (5) kati ya saba huku Tanzania Prisons akiibuka na ushindi kwenye mitanange miwili tu tena kwa ushindi unaofanana wa goli moja kila mchezo waliopata ushindi pamoja na kushuhudia sare kwenye mchezo mmoja baina yao.

Uzuri ni kuwa michezo yote waliyokutana tokea 2020 imezaa magoli huku jumla ya magoli 18 yakifungwa na timu zote hata hivyo Simba SC wamefanikiwa kufunga jumla ya magoli 13 kati ya hayo na Tanzania Prisons akifunga magoli 5 tu na kati ya hayo magoli mawili yalifanikiwa kuwapa alama 6, ambapo 2020/2021 waliibuka na ushindi wa 1-0 wakiwa nyumbani pamoja na msimu wa 2021/2022 wa kuibuka tena na ushindi wa 1-0 nyumbani huku wakifunga goli moja kwenye sare ya 1-1 msimu wa 2020/2021 ugenini na magoli mawili waliyofunga wakifunga walipopoteza 7-1 ugenini nakwenye msimu wa 2022/2023  3-1 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza msimu huu.

Ndani ya michezo mitatu ya mwisho takwimu zinampa nafasi kubwa Simba SC kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo ambapo ndani ya michezo hiyo ameibuka na ushindi mfululizo huku akifunga magoli 11 na akiruhusu magoli mawili.

Tanzania Prisons wamebadilika sana kiucheza kwenye msimu huu wamekuwa wakicheza mpira wa kuvutia sana tokea kikosi hicho kuwa chini ya Kocha Ahmad Ally, wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-4-2 ambapo muda mwingi mashambulizi yao yake kuwa yakianzia nyuma kwa walinzi kwenda mbele muda mwingi wa mchezo wamekuwa wakiweka mpira chini na kutengeneza nafasi kupitia winga na wakati mwingine kupitia katikati huku silaha yao kubwa ikiwa ni eneo Lao la kiungo na kwenye kutengenza magoli wakimtumia zaidi Zabona Hamis Mayombya, Kibaya ni kuwa namna ya uchezaji wao wakikutana na timu yenye kasi pembeni na viungo wanaopiga mipira ya pembeni wanapata shida.

Upande wa Simba SC wamekuwa hawana kiwango cha muendelezo kwa msimu huu licha ya kupata ushindi kwenye michezo yao, silaha yao kubwa kwa sasa ni kiungo wao Saidi Ntibazonkiza kutengeneza magoli na kusaidia kukaba kuanzia juu jambo ambalo limemfanya kuwa kati ya wachezaji wa kumchunga unapokutana na Simba SC. Mfumo wa 4-2-3-1 umekuwa moja ya mifumo wanaoutumia zaidi huku wakibadilika Mara kadhaa hadi kwenye 4-3-3 kwa kutumia zaidi eneo la pembeni kuingia kati. Tokea mzunguko wa pili umeanza imekuwa ngumu kwao kudondosha alama na wachezaji wao wengi wamekuwa na kiwango bora sana na kitu ambacho kimewafanya kuruhusu magoli machache.

Kitakwimu za wao kwa wao nafasi kubwa anapewa Simba SC kuibuka na ushindi na hiyo ni kutokana na kuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yao ya mwisho kwa kushinda yote na kufunga magoli 11, hata hivyo ubora na namba Ya uchezaji wa sasa wa Tanzania Prisons unafanya kuweka matarajio ya kushuhudia mchezo mzuri wenye mbinu na Ufundi kutoka kwa wachezaji wa timu zote mbili.

SOMA ZAIDI: Barua Kwako Mwanamfalme Prince Dube

1 Comment

  1. Pingback: Simba Waliichukulia Poa Prisons Wameadabishwa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version