Ni mchezo wa Saba kwao kukutana kwenye Ligi kuu Soka Tanzania bara (Ligi kuu ya NBC) tokea timu hizo zianze kukutana, mchezo wa Leo utakuwa ni mchezo wa nane kwa timu hizo kukutana.

Takwimu za michezo hiyo Saba waliyokutana Simba SC imefanikiwa kushinda michezo yote huku kikosi cha Dodoma Jiji FC wakiwa hawajafanikiwa kushinda mchezo hata mmoja kati ya michezo hiyo. Hata hivyo Simba SC imefanikiwa kufunga magoli 14 huku wakifungwa au Dodoma Jiji FC wakifunga magoli 2 pekee kati ya michezo hiyo Saba.

Kitu cha tofauti ni kuwa katika michezo yao waliyokutana, michezo mitano Ya mwisho kikosi cha Dodoma Jiji FC hakijafanikiwa kufunga goli lolote lile huku wakiruhusu kufungwa magoli tisa (9).

Upande wa Ligi kuu ya NBC msimu huu mpaka sasa Simba SC anashika nafasi Ya tatu na alama 57 huku Dodoma Jiji akishika nafasi Ya 11 akiwa na alama 30, katika michezo yao mitano Ya mwisho kwenye Ligi Simba SC amefanikiwa kushinda michezo 3 na kutoa sare michezo miwili (2) na akifunga magoli 10 na akiruhusu magoli matatu tu (3).

Dodoma Jiji FC wao kwenye michezo mitano wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja wakitoa Sare michezo 3 na kufungwa mchezo mmoja tu, hata hivyo wamefanikiwa kufunga goli moja na kuruhusu magoli 2 tu.

Namna matokeo Ya michezo yao mitano yalivyo basi ni dhahiri kuwa timu zote zimekuwa vizuri kwenye eneo la kuzuia katika michezo 5 ya mwisho kwani ni magoli matano tu kwa pamoja wameruhusu, tofauti ni kwenye eneo la ushambuliaji ambapo Simba SC wanaonekana wakiwa vizuri tofauti na Dodoma Jiji ambao wamefunga goli moja tu jambo linalotia shaka uhatari wa eneo Lao la ushambuliaji kuelekea mchezo huo.

Simba SC wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kulingana na unitaji wa mchezo huo kwao kwani utawafanya kujiweka kwenye nafasi nzuri kumaliza nafasi Ya pili kwenye Ligi msimu, pili ni Hamasa Ya kikosi hicho kwa sasa sehemu kubwa ya wachezaji wameonyesha kujituma zaidi japo changamoto ni eneo Lao la mwisho wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi ila wamekuwa wakitumia chache zaidi Ya zinazotengenezwa. Ukosefu wa Kiungo wao Clatous Chama imekuwa pengo kubwa kwenye kikosi hicho kwani ndiyo Mchezaji ambaye amekuwa na usahihi mzuri kwenye kutengeneza nafasi na kutumia nafasi chache anazopata kufunga goli.

Kikosi cha Dodoma Jiji FC changamoto yao kubwa pia ni kutumia nafasi wanazopata kwenye eneo lao la mwisho la ushambuliaji nafasi nyingi zimekuwa hazitumiwi vizuri na ilo linajionyesha katika michezo 5 ya mwisho wamefunga goli moja pekee.

Hivyo kwa namna takwimu zilivyo kwa pande zote mbili kuna nafasi kubwa ya kushuhudia mchezo mzuri kwani timu zote mbili zinasifa Ya kufunguka kushambulia na siyo kukaa nyuma kuzuia zaidi tofauti kubwa ni Simba SC wakiwa na uhatari zaidi eneo la kati pamoja na pembeni kwenye kutengeneza mashambulizi ila kwa upande wa Dodoma Jiji wao wamekuwa na uhatari pembeni mwa uwanja kuliko katikati mwa uwanja.

SOMA ZAIDI: Je Simba Na Azam Wana Nafasi Ya Kumzuia Yanga Msimu Ujao?

3 Comments

  1. Sema semba anatakiwa akaze sana laa sivyo! Hatoboi kuwa msindi wa pili maana hata Azam amepania sana kwahiyo hii ni vita mraa

    Tajiri Abaaas

  2. Luhinda Luhinda on

    Kama dodoma watapata goal dkak za mwanzon bx shughul itakuwa imeisha maaan Dodoma wanaweza waka defense zaid

Leave A Reply


Exit mobile version