Msimu wa kwanza wa Ronaldo nchini Saudi Arabia ulifikia tamati Jumatano iliyopita, ingawa mshambuliaji huyo nyota hakuwepo wakati Al-Nassr iliposhinda Al-Fateh 3-0 na kumaliza nafasi ya pili katika ligi. Alisema Ronaldo “Nina furaha hapa, nataka kuendelea hapa”

Nyota wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo, alithibitisha katika mahojiano na Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwamba “ataendelea na timu” msimu ujao.

“Nadhani ligi ni nzuri sana lakini nadhani bado tuna fursa nyingi za kukua. Nadhani ligi ni nzuri, ni ya ushindani. Tuna timu nzuri sana, tuna wachezaji Waarabu wazuri sana. Miundombinu nadhani wanahitaji kuboresha kidogo zaidi. Waamuzi na mfumo wa VAR. Nadhani wanapaswa kuwa haraka kidogo. Mambo madogo mengine wanahitaji kuboresha. Lakini mimi nipo furaha hapa, nataka kuendelea hapa, na nitaendelea hapa,” alisema alipoulizwa kuhusu uzoefu wake wa kucheza katika ligi hiyo.

“Na kwa maoni yangu, ikiwa wataendelea kufanya kazi wanayotaka kufanya, basi katika miaka 5 ijayo nadhani Ligi ya Saudi inaweza kuwa ya tano (ligi bora) duniani,” aliongeza.

Ronaldo akiwa amethibitisha nia yake ya kuendelea nchini Saudi Arabia, akisema yeye na familia yake wanafurahia maisha katika Ghuba, tetesi za usajili bado zinaendelea kuhusu uhamisho wake kwenda moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya na inatarajiwa kuendelea kwa kipindi chote cha majira ya joto.

Msimu wa kwanza wa Ronaldo nchini Saudi Arabia ulifikia tamati Jumatano iliyopita, ingawa mshambuliaji huyo nyota hakuwepo wakati Al-Nassr iliposhinda Al-Fateh 3-0 na kumaliza nafasi ya pili katika ligi.

Ronaldo, ambaye alijiunga na klabu ya Riyadh mwezi Desemba na kufunga mabao 14 katika mechi 16 za ligi, alipata jeraha la misuli siku nne kabla na akapumzika kabla ya mechi za kufuzu kwa Mashindano ya Ulaya ya Ureno dhidi ya Bosnia-Herzegovina na Iceland mwezi Juni.

Soma zaidi: Habari zaidi kama hizi hapa 

Leave A Reply


Exit mobile version