Chelsea ‘The Blues’ wamelenga kumsajili kiungo hatari wa Celta Vigo, Gabri Veiga, na huenda wakamuuza Kai Havertz baada ya kupata taarifa kuwa mshambuliaji Mjerumani anataka kuondoka, kulingana na The Guardian.

Mauricio Pochettino anakabiliwa na kazi kubwa ya kujenga upya kikosi chake baada ya kuwa kocha mkuu na anaweka kipaumbele katika kuongeza wachezaji katika eneo la kiungo, huku pia wakitaka kipa na mshambuliaji.

Veiga ameibuka kuwa mmoja wa viungo bora vijana barani Ulaya na mkataba wake una kifungu cha kumnunua cha Euro milioni 40 (£34.4m).

Liverpool na Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini Chelsea ‘The Blues’ wapo tayari kupambana kwa nguvu kumsajili.

Havertz amekuwa katika mipango ya Real Madrid, ambao wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Bayern Munich.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema kuwa anataka changamoto mpya. Ana miaka miwili kwenye mkataba wake na inaonekana hataongeza muda wa mkataba huo.

Inaeleweka kuwa Chelsea watadai pauni milioni 75 kwa Havertz.

Kwa taarifa zaidi za usajili tufatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version