CHASAMBI HUYOOO MSIMBAZI , BENCHIKHA APIGILIA MSUMARI USAJILI WAKE MSIMBAZI

Moja kati ya stori kubwa inayozungumzwa katika vijiwe vya soka mtandaoni nchini Tanzania ni pamoja na kuelekea usajili wa dirisha dogo la januari kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Ladaki Chasambi anayekipiga Mtibwa Sugar ni miongoni mwa mastar wanaotajwa kuwa tayari amemalizana na klabu ya Simba kwa ajili ya kuwatumikia wekundu wa msimbazi kuanzia dirisha la januari.

Chasambi ni moja kati ya wachezaji ambao amepandishwa msimu huu kutoka timu ya vijana ya U20 ya Mtibwa Sugar inayoshikilia ubingwa wa Ligi ya umri chini ya miaka 20 kwa msimu wa tano mfululizo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Mtibwa zimefichua kuwa klabu ya Simba imekubali kununua mkataba wa miaka miwili aliokuwa nao Chasambi na klabu ya Mtibwa, kisha fasta ikamalizana na Mchezaji Bora huyo wa U20 2023 ili dirisha likifunguliwa tu aanze kukinukisha Msimbazi.

Leave A Reply


Exit mobile version