Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa klabu umewasimamisha wachezaji Nassor Kapama na Clatous Chota Chama kutokana na vitendo vya Utovu wa nidhamu.

Kupitia katika mitandao ya kijamii ya wekundu hao wa msimbazi imetangaza kuwasimamisha wachezaji hao na watapelekwa katika kamati ya nidhamu kwa hatua stahiki zaidi za kinidhamu. Uongozi wa klabu ya Simba umeendelea kwa kuwakumbusha watumishi wake wote kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitasita kumchukulia hatua yeyote atakethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo. Endelea kusoma zaidi kuhusu taarifa za ligi kuu kwa kuboinyeza hapa.

Barua ya klabu ya Simba kuhusu kumsimamisha Chama na Kapama
Leave A Reply


Exit mobile version