Wakati ambao Ibrahim Ajibu anaibuliwa na Simba SC ilikuwa ngumu kuamini kuwa anaweza kufanya makubwa na Kiwango bora, lakini jambo kubwa kwa klabu ya Simba SC ni Imani kubwa kwake na kwa vijana wenzake kutoka timu zao za vijana.

Alidumu kwa muda mrefu sana na Simba SC kiwango bora, ufundi na kujituma kiwanjani, ilifika hatua akaimbwa na mashabiki na wapenzi wengi nchini bila kujali upande wowote ule anaocheza mchezaji huyo.

Ilifika hatua Ibrahim Ajibu akabatizwa majina yaliyokuwa yanaendana na namna anavyocheza, sikushangaa alipopewa Jina la “Mwamba wa makororo” wengi waliamini kuwa ndiyo mchezaji pekee aliyekuwa na ufundi mwingi nchini kwa kizazi chao.

Kuna msemo maarufu aliyowahi kuusema kipa wa Simba SC Aish Salum kuwa “Mchezaji bora anachukua mataji”, ukame na ugumu wa kuchukua makombe kwa miaka yake ya ubora ndani ya Simba SC yalimpa hamasa na kuamia upande wa pili kwa ajili ya kuchukua na kubeba makombe.

Na nikukumbushe kuwa wakati anaondoka Simba SC upande wa pili ulikuwa bora sana na walichukua makombe yote makubwa nchini huku upande wa Mnyama akijitafuta na kuunda kikosi kipya kwa ajili ya kufanya makubwa baada ya muda mrefu na ndiyo wakati ambao waliunda timu bora sana kiwanjani.

Alipojiunga tu na Yanga SC ni kama aliama na ukame wa makombe aliyokuwa akiyatamani wakati Yanga SC akinyanyua na yeye akiwa upande wa pili, ni kama alipishana na mafanikio na msimu ambao anatangazwa Yanga SC ndiyo msimu ambao Mnyama akanyanyua makombe makubwa nchini, licha ya kiwango bora sana Jangwani ila aliambulia patupu kwa misimu miwili na kuamua kurejea Simba SC na alichukua makombe bila ya kuwa na kiwango bora ambacho alionyesha kabla na baada ya kuondoka unyamani.

Wacha nikurejeshe tena hapo hapo Simba SC, 2018 walimtambulisha Kiungo Clatous Chama akitokea kwao Zambia huku akiwa Hana Jina na umaarufu wowote ule wa kisoka kwa kiwango kikubwa nchini kwao, ila kikubwa kwa Simba SC ilikuwa ni Imani kwake kama ambavyo walifanya kwa kijana wao mwenyewe waliyemuandaa.

Ilimchukua msimu mmoja tu kuonyesha ubora wake, watu wa mpira nao wakaanza kumpa jicho la pili na la tatu kuona uhalisia wa kiungo huyo, msimu uliyofuata ni kama Imani ikaanza kulipa ufundi, udambwi udambwi na ubora wa Clatous Chama ukaonekana na hapo ikawa wakati rasmi kwa wapenzi, mashabiki na watu wa kimpira kumuimba Fundi huyo ambaye alikiwasha sana na kuwa tegemezi.

Utulivu ndiyo ilikuwa silaha yake kiwanjani akili ya kimpira iliambata naye awapo kiwanjani. Ilifika wakati wa kumuheshimisha na jambo kubwa ni kupewa majina mbalimbali ambayo yaliaakisi kile alichokuwa akikifanya kiwanjani.

Nikuambie tu hata mimi sikushangaa alipoitwa “Mwamba wa Lusaka” au “Brain ya mpira” ni kama mashabiki na wapenzi wa mpira nchini walimbatiza majina ambayo yalikuwa yanaendana na kile mchezaji alichokuwa akikifanya kiwanjani.

Baada ya muda mrefu wa kuchukua makombe akiwa na Simba SC, ukame ukaanza ndani ya timu hiyo na baada ya muda Kumbukizi ya Ibrahimu Ajibu na Simba SC ikaonekana kwa Clatous Chama, sinema ambayo Ajibu aliifanya Chama naye ameirudia, wakati ambao Ibrahimu anaondoka Simba ilikuwa hawajachukua makombe na wakati ambao Chama anaondoka Simba nao pia wana muda hawajachukua Makombe.

Akili yangu bado imebaki inawaza na kufikiria kuwa kile kilichotokea kwa Ibrahim Ajibu kinaweza kutokea tena kwa Clatous Chama? Lakini nakumbuka kuwa ubingwa unaamuliwa kiwanjani na baada ya msimu kutamatika tunampata bingwa kati ya wengi. Basi na mimi nikajisemea mwenyewe tu kuwa Wacha niache nafasi na muda utaongea kunipa majibu ya maswali yangu kati ya kurasa hizo mbili tofauti.

SOMA ZAIDI: Hatukatai Umefanya Vingi Ila Hili Ni Deni Kubwa Sana Kwako

10 Comments

  1. Jjb-hsnf-fdk on

    Sawa lakn kusema kwamba chama anapishana na makombe hapo sio kweli
    Wakati mwingine haiitaji kukariri na kuamin yaliyopita mim naamin
    Simba kuchukua ubingwa
    Bado sana.

  2. Ukiangalia kwa nadharia unawez ukasem yanaweza chama kumkuta ya ajibu ila mpira haukaririki inawez ikawa tofaut

  3. Pingback: Ni Ngumu Kuamini Kamwe Unaondoka Jangwani

Leave A Reply


Exit mobile version