Kabla ya kuanza kwa michuano ya mataifa barani Afrika kulitoka moja kati ya taarifa iliyoibua maswali mengi sana kwa mashabiki wa soka Tanzania taarifa ambayo ilitoka katika klabu ya Simba kuhusu wachezaji wao kadhaa kusimamishwa na mmoja wao akiwepo kiungo wao Clatous Chota Chama raia wa Zambia.

Baada ya taarifa hiyo mengi yakaibuka ambapo kila shabiki akawa na maoni yake kuhusu Sakata la kusimamishwa wachezaji hao akiwemo Chama, wapo ambao walisema ni wakati wake kuondoka tu kwani kumekua na mengi yanayotokeaga kumhusu yeye inapofikaga wakati wa usajili lakini wapo pia ambao wakaona si sawa viongozi wake na kuyamaliza.

Katika AFCON, Chama akapata nafasi katika kikosi cha Zambia na kucheza mchezo mmoja dhidi ya Tanzania ambapo alitoa assist ya bao la kusawazisha lakini sasa jambo likaibuka upya baada ya Zambia na Tanzania kutolewa na ni wakati sasa ambao ligi inarejea na Simba wana mechi ngumu mbeleni.

Taarifa ya kusamehewa Chama na kurejeshwa katika kikosi cha Simba kuna mengi yanakua kichwani kwangu na kujiuliza mengi sana kwanza ni kuona namna ambavyo uongozi wa simba ulivyo haswa kukitokea mambo kama haya yanayoitwa Utovu wa nidhamu kwa wachezaji utagundua kuwa klabu ya Simba viongozi wake ni dhaifu sana mwanzo walisema mchezaji ameikosea klabu halafu wao ndo wanamuomba radhi?

Tunapaswa kuona namna ambavyo klabu ya Yanga hufanya maamuzi kwenye masuala kama haya wale hawana muda hata kidogo umezingua wanakutoa katika klabu yao wamesimamia misingi yao kabisa unajua Chama hatocheza milele itafika wakati ataondoka, jiulize tunatengeneza nidhamu gani kwa wengine?

Vitu vingine ni vya ajabu sana na viongozi wa Simba wana uswahili, katika barua mansema mmemsamehe ina maana kweli alikuwa anahujumu timu halafu mkaona mumsamehe au hamjamkuta na hatia hiyo mmeona bora muendelee au ni hela ya kuvunja mkataba mmekosa,au mnaogopa atachukuliwa na wenzenu au?

Kauli hizi ni wazi zinadhihirisha kuwa kutokana na mambo ambayo huwa yanatokea baina ya Simba na Chama, viongozi wa klabu wanatakiwa kujitathmini.

SOMA ZAIDI: Inonga Amejiuza AFCON Sitashangaa Akiondoka Simba

 

2 Comments

  1. Pingback: Ligi Kuu Imerejea Marefa Kuweni Na Msimamo - Kijiweni

  2. Pingback: Unajua Kwanini SIMBA Ni Muhimu Kushinda Hii Leo? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version