Maisha yanabadilika haraka sana wakati timu kama Tanzania bado zikijikongoja kwenye maendeleo ya mpira miaka 10 iliyopita kule South Africa nchi yenye raia wasiozidi laki 7 kwa ilikua na hadithi ya kushangaza baada ya kufika robo fainali bila kutegemewana wengi kabla ya kuondolewa na Ghana ya akina Asamoah Gyan.

Miaka 10 baadae Cape Verde taifa dogo zaidi kati ga timu zote zinazoshiriki michuano ya Afcon mwaka huu wamekua timu ya kwanza kufuzu hatua ya mtoano (hatua ya 16) wakiwa kwenye kundi gumu lenye miamba Ghana na mabingwa wa kihistoria wa michuano hio Misri.

Mafanikio ya Cape Verde hayajaja kibahati tu ni mwendelezo wa kile walichoamua kukifanya miaka kadhaa iliyopita, ni ngumu kuamini kuwa walifuzu michuano yao ya kwanza Africa mwaka 2013 kabla ya kuondolewa na Ghana katika hatua ya robo fainali, tangu hapo hawakuwahi kurudi nyuma wakienda kufuzu pia michuano ya 2013, 2015, 2021 na mwaka huu.

Mwaka 2000 Cape Verde walikua wanashika nafasi ya 182 duniani lakini leo hii wanashika nafasi ya 73 huku mwaka 2014 wakipanda mpaka nafasi ya 27 duniani je, unadhani mataifa mengine yanafeli wapi? Wachezaji wengi wa nchi yao huiweka timu mbele kwanza badala ya ubinafsi uwanjani wala kumtegemea mchezaji mmoja awape matokeo na hivyo kupelekea kupata matokeo chanya uwanjani kwa mfano magoli yote 8 waliyoyafunga wakati wa kufuzu michuano yam waka huu yalifungwa na wachezaji 8 tofauti.

Mpaka mwaka 1998 Cape Verde hawakua na viwanja vya mpira vya nyasi lakini kwa sasa wana viwanja Zaidi ya 25 baada ya kutemebelea fursa ya project za FIFA za viwanja kwenye ngazi za chini hali iliyochangia kukuza soka lao ngazi ya vijana licha ya udogo wa taifa lao lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4,033 tu.

Licha ya kutumia wachezaji wengi wa kigeni wenye asili ya nchi hio wanaocheza soka ulaya lakini taifa hilo limeamua kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya soka la vijana huku baadhi yao wakipata nafasi katika shule za mpira katika nchi za Ulaya kama vile Ureno.

Moja ya mafanikio makubwa kabisa katika soka la Cape Verde ni chama cha soka cha nchi hio kuamua kuwekeza kwenye kuwashawishi wachezaji wengi wa nchi hio waliozamia nchi za ulaya kutafuta mafanikio ya kimpira  au kuwa na asili ya Cape Verde kuchagua kuichezea timu yao ya Taifa mfano mzuri ukiwa ni nyota wa zamani wa Manchester United Bebe aliyeamua kukubali wito wa kuichezea nchi hio ya asili ya mama yake mwaka 2022.

Miaka ya nyuma muamko wa taifa hilo kisoka ulikua chini na hivyo kukosa fursa ya kuwashawishi wachezaji wengi wenye asili ya nchi hio wanaocheza Ulaya kuchezea taifa hilo huku Patrick Viera, Luis Nani, Patrice Evra na Henrik Larson wakiwa ni baadhi ya wachezaji waiokua wanafuzu kuichezea nchi hio lakini hakukua na jitihada zozote za kuwashawishi.

Leo hii nchi hio imewekeza kwa maskauti wanaozunguka kwenye nchi mbalimbali za ulaya hasa Ureno kutafuta wachezaji wenye asili ya nchi hio amba oleo hii wanaisaidia nchi hio kufanya vizuri katika soka la Africa.

Je, sisi wengine tunafeli wapi? Nadhani ni nafasi sahihi kwa viongozi wetu kwenda kufanya research katika nchi hi ndogo yenye watu laki 6 ili kujifunza mbinu za nini kinapswa kufanyika katika nchi yetu ili kuleta mapinduzi ya mpira hasa uwekezaji katika soka la vijana nanamna ya  kutafuta wachezaji wenye asili ya Tanzania wanaocheza nje ya nchi.

SOMA ZAIDI: Huu Hapa Mkeka Wa Kumpiga Mhindi Leo

1 Comment

  1. Pingback: Kilichotokea AFCON Kwa Mataifa Makubwa Ni Somo - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version