Klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi viingilio vya mchezo utakaowakutanisha Simba dhidi ya Wydad katika dimba la Benjamin Mkapa tarehe 19. Taarifa hiyo kutoka kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally anasea kuwa mechi dhidi ya Wydad ni lazima kushinda kwani hakuna option nyingine waliyonanyo kwa sasa na wataweka rehani roho zao.

“Mechi ya Kagera Sugar ni maandalizi ya mechi dhidi ya Wydad na tiketi zake zitaanza kuuzwa kesho. Mechi dhidi ya Wydad itakuwa tarehe 19 Desemba, 2023 saa 10:00 jioni na tutaingia tukiwa na option moja tu, kushinda. Tutaweka rehani roho zetu ili kushinda.” alisema Ahmed Ally.

Katika mchezo huo viingilio vitakua Mzunguko ni Tsh. 5,000 huku VIP C – Tsh. 10,000 lakini pia VIP B ikiwa Tsh. 20,000,VIP A – Tsh. 30,000 na zile Tiketi za Platinum zikiwa ni  Tsh. 150,000.”

Aidha Ahmed amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi zaidi ili kufanikisha jambo hilo na kutinga robo fainali “Kufika robo fainali tutafanikisha kwa kila Mwanasimba kuhusika kwa kuja uwanjani. Malengo yetu ni nusu fainali na itakuwa aibu kubwa sana tusipofika robo fainali. Na Simba ya sasa nyie wenyewe mnaiona, timu ina mabadiliko makubwa.”

Lakini pia kama ilivyo kawaida ya klabu ya Simba, kuelekea mchezo huo dhidi ya Wydad mwalimu wa klabu hiyo  ndiye atakua mgeni rasmi wa mechi

“Mgeni rasmi atakuwa mwalimu Abdelhak Benchikha ‘GENERAL’. Yeye ndio tumempa hadhi hiyo. Huyu ndio kocha bora wa Afrika kwa vilabu na kocha wa tatu kwa ubora Afrika lakini pia ni mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika tukiwa nyumbani na sababu kuu ni mabadiliko ambayo ameyaleta .Huyu ni kocha mkubwa sana Afrika, Wanasimba tujivunie tukiwa ba kocha Abdelhak Benchikha. Ndugu yangu Mwanasimba na wewe hakikisha unaandika historia siku hiyo kuwepo uwanjani.”- Ahmed Ally.

Endelea kusoma taarifa zetu mbalimbali pamoja na makala za kusisimua kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version