Kocha wa Singida Fountain Gates FC (Zamani Singida Big Stars), Hans van der Pluijm amemwagia sifa kiungo wake, Bruno Gomes raia wa Brazil kwa kusema licha ya ugeni wake Tanzania na Afrika amethibitisha ubora kiasi cha kumezewa mate na klabu za Simba na Yanga.

Mara baada ya msimu kumalizika Pluijm alimtaja kiungo huyo kuwa ndiye mchezaji wake bora kwenye kikosi chake cha Singida BS ambacho kinatiketi ya msimu ujao kushiriki michuano ya kimataifa kufuatia kumaliza ndani ya nafasi nne za juu.

Pluijm anakiri kikosi chake kuwa na wachezaji wengi wazuri ambao wamefanya kazi kubwa kwa msimu uliopita lakini Bruno Gomes alifanya zaidi ya kawaida.

“Unajua hii ni mara yake ya kwanza kucheza Afrika, hakuwa akijua aina yetu ya mpira  ulivyo lakini ameweza kuendana na sisi na kutupa kilicho bora,”

“Wapo wachezaji wengi ambao wamekuwa wakija Afrika lakini utofauti na mazingira huwafanya kuhitaji muda wa kuzoea, ila Bruno amekuwa akizoea bila ya kuathiri utendaji wake, ” alisema Pluijm.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga na Azam FC aliendelea kumuongelea kwa kusema,”Naamini kuwa bado yupo na vitu vingi vya kutuonyesha, ni kati ya wachezaji ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu.”

Bruno Gomes ambaye ni mfungaji bora wa Singida BS akiwa na mabao 10 kabla ya kuja Tanzania na Afrika ambapo hii ni mara yake ya kwanza, alikuwa akiichezea River Atletico ya nchini kwao, Brazil.

Kwa taarifa zaidi za michezo, tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version