Bila njia hakuna kwenda,bila ukweli hakuna kujua,bila uzima hakuna kuishi. Ukweli na uzima ni muhimu, Kusifiwa kusingetuletea shida kama tusingekuwa tunajisifu sisi wenyewe badala ya kusubiri kusifiwa. Kusifu ni kutoa maelezo mazuri juu ya mtu au jambo fulani.

Pale Hispania kuna kikundi kinaitwa Biris Norte hiki ni kikundi cha ushangiliajia katika klabu ya Sevilla ya nchini Hispania na ndio kikundi maarufu zaidi kwenye klabu hiyo.Kilianzishwa mwaka 1974 kikijulikana  kwa jina la Biri Biri la Peña.

Katika msimu wa 1974-1975, wakati wa mechi kati ya Sevilla na Cádiz, kundi la vijana lilikuwa na bendera iliyosoma “Peña Biri-Biri” likishangilia kwa shangwe kubwa. Hatimaye Sevilla ilishinda na goli likifungwa na  Alhaji Momodo Njle, anayejulikana kama Biri-Biri, na kikundi hicho kilipaza sauti za kuimba za “Biri-Biri!” na kupiga ngoma.Walipokea sifa nyingi kutoka kwa mashabiki wengine wa Sevilla. Biri-Biri ilipaswa kufadhiliwa mara nyingi na wanachama wenye nguvu kutokana na ushawishi wao kiushangiliaji

Kundi hilo ni muunganiko wa makundi ambao sasa una watu zaidi ya 1000.

Katika soka la Tanzania wengi tunapenda zaidi kusifu na sio kukosoa na kushauri. Inahitaji moyo wa ujasiri haswa kuikosoa Yanga Sc au Simba Sc lakini ni furaha kubwa pale utakapowasifia hata kama hapahitaji sifa.

Jioni ya tarehe 8 September 2019 nilikuwa miongoni mwa Watanzania ambao walikuwepo uwanjani kushuhudia Tanzania ikiitupa nje Burundi, dakika za mwazoni hakukuwa na amsha amsha kubwa sana kiasi kwamba hata wachezaji nao kama walisizia. Tanzania na Burundi zikaenda dakika 120 katika dakika 15 za kwanza kwenye 30 hakukuwa na shangwe lakini katika dakika 15 za mwisho ni kama Watanzania tuligeuka walevi wa Kijeruman na Urusi.

Mtanisamehe kwa huo mfano mashabiki wa Ujerumani na Urusi huwa wanakuwa na amsha sana timu zao zinapocheza lakini muda huo tayari vichwa vinachemka kidogo. Ilikuwa hivyo kwa Watanzania shangwe la nguvu lilipigwa katika hizo dakika hakukua na staa au stara hata Harmonize aliamua kujipa uchizi kidogo wa kimpira,naam ilikuwa ni tafsiri halisia sasa ya mashabiki.

Kuanzia August timu zetu zitaanza kutupa karata zao katika michuano ya kimataifa yaani klabu bingwa na Shirikisho pia ambapo Simba sports club na Coastal Union zipo Shirikisho wakati Young Africans sports club zipo klabu bingwa.

Kwa asilimia kubwa mashabiki wa timu zetu huwa kama wamelala wakati vijana wao wakiwa wanapambana uwanjani mara nyingi wale ambao wanakuwa wapo pale huwa wamepoa ni wachache wenye amsha ya kutosha zaidi.

Sitaki niwasifie ila nawapongeza tu kupenda timu zenu lakini kuelekea michezo hiyo sasa amkeni mtambue mpo kimataifa, wachezaji wanahitaji kelele zenu. Nasikia kuna kamati za hamasa binafsi sioni umuhimu wake sana katika hizo kamati ni kupoteza pesa tu kuwalipa japo Mh. Zungu alitamka hakuna mpira wa kujitolea kwa sasa.

Kamati kubwa ya hamasa kwangu mimi ni katika matawi yenu,ni katika makundi yenu ya WhatsApp huko, Kuna umoja wa matawi,kuna umoja wa makundi ya WhatsApp viongozi mnapaswa kuhimiza watu wenu katika hayo makundi na matawi waende uwanjani na kwakuwa mnajiita wamoja basi mkakae sehemu moja na kuonyesha umoja wenu kwa kushangilia mwanzo hadi mwisho.

Ni wazi kwamba umoja huo upo kama jina tu kwa sababu matawi na hayo makundi yao mengi yameundwa baada ya mifarakano hakuna umoja ule unaohubiriwa mara kwa mara na ndio maana hata uwanjani wamegawana sehemu za kukaa ilihali wapo timu moja wote, lakini kuelekea katika michezo ya kimataifa wanapaswa kusahau na kuungana vilivyo wakakae pamoja ikiwezekana hata matambara yao yapangwe pamoja na kushangilia bila kupumzika.

Kuna ugumu kiasi chake kufanya hivyo lakini kwa kuwa waliamua kuwa na umoja basi tuonyesheni kuanzia sasa na kuweza kuwaziba wapizani, Natambua kabisa viongozi wenu wanahimiza kuwa wamoja basi unganeni nao katika hilo

Umoja wa Matawi na makundi ya WhatsApp hii ni kazi yenu kuunganisha mashabiki na kuamsha bila kuchoka zile ngoma ambazo hupigwa basi zipigwe katika sehemu moja kwa hamasa zaidi.

Itakuwa ni kazi bure kuujaza uwanja halafu kukawa kama hakuna mashabiki,kuujaza katika mechi zenu huko kimataifa kuendane na kushangilia pia.

Kila lenye heri kwenu katika uwakilishi wenu huko kimataifa.

SOMA ZAIDI: Udhaifu Na Ubora Wa Yanga Kwenye Mifumo Hii Kiwanjani

2 Comments

  1. Pingback: Hakuna Simba Na Yanga Bila Msingi Wa Uwepo Wao

  2. Pingback: Ratiba Kamili Ya Mechi Za Awali Ligi Ya Mabingwa Afrika 2024/25

Leave A Reply


Exit mobile version