Wakati bado mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wakiendelea na kusheherekea kutinga hatua ya robo fainali kwa kumfunga mwarabu bao 4 saaafii basi niwakumbushe tu unaposherekea ushindi wa Yanga kuingia robo fainali ya klabu bingwa Afrika tuwakumbuke wekundu wa msimbazi yaani klabu ya Simba nao.

Tusiache mbachao kwa msala upitao kwani klabu ya Simba ilichonga njia kwa machozi na damu kutuonesha ya kwamba inawezekana kushindana na timu zenye misuli mikubwa kibajeti na kimfumo za kaskazini na baadhi za kusini ndipo timu zingine za Tanzania zikaanza kuamka ikiwemo Yanga,Azam fc na Namungo,

Nimeona mijadala mingi ikiendelea na kuonesha dharau kwa miamba hiyo ya Tanzania inayoongoza mabadiliko chanya ya kisoka kila uchwao na wengine kuigiza au kuboresha,ama hakika kila mwanasoka anapaswa kusema shikamoo simba kwa maana sasa ushindani utaongezeka na hatimae kombe la Afrika litaletwa nchini.

Wengine mara kwa mara tumekuwa tunajitahidi kusema ukweli na kuwapa maua yao hawa Yanga toka msimu huu unaanza.Ni ukweli ulio wazi kuwa Yanga inacheza mpira wa kueleweka, ni timu yenye kasi na inaweza kulazimisha ushindi pale mambo yanapokuwa magumu.

Pamoja na kwamba kuna mara kadhaa katika ligi ya NBC ni kama ilibebwa kiaina mfano katika ile game ya Kagera Sugar ila “overall” hauwezi kubeza uwezo na kiwango ambacho wamekionyesha. Naona kabisa hata kama wangepata ushindi mwembamba dhidi ya CR Belouizdad, Yanga ilikuwa na uwezo wa kwenda kulazimisha sare au hata ushindi katika mechi dhidi ya Al Ahly.

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga

 

Leave A Reply


Exit mobile version