Kocha mkuu wa wekundu wa msimbazi yaani klabu ya Simba Abdelhak Benchikha ni miongoni mwa makocha wenye CV kubwa barani Afrika lakini pia na uzoefu ukichangiwa na uwezo mzuri wa kufundisha soka pia ni miongoni mwa makocha wasio wavumilivu wa nyakati ngumu katika kazi yake.

Ukitazama kipindi hiki ambacho klabu ya Simba inapitia, kinafanya nikumbuke baadhi ya maamuzi magumu ambayo amekua akiyafanya na kuwa kama mmoja ya makocha mbao sio wavumilivu wanapokua katika majukumu yao.

Tunapoelekea katika mechi ya watani nakumbuka tukio la mchezo wa mwisho ambapo Simba walipata sare dhidi ya Ihefu na dakika ambazo kocha huyu alikaa akitafakari baada ya mchezo kuisha wakiwa hawajapata ushindi katika mechi zao 4 mfululizo za michuano yote.

Moja wapo ya maamuzi magumu kuwahi kuyachukua ni mwaka 2011 akiwa kama Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Algeria, alichukua alijiuzulu baada ya kufungwa mabao manne na timu ya Taifa ya Morocco katika mwendelezo mbovu wa matokeo katika timu yake hiyo.

Mwaka 2023 akiwafundisha USM Alger, licha ya mafanikio makubwa aliyoyapata klabuni hapo ikiwemo kutwaa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga, alijiuzulu kuifundisha Klabu hiyo kutokana na tukio la kuzomewa na mashabiki wakati na baada ya mechi kuisha Katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu Algeria.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Yanga, nini kitatokea, ni suala la muda na kusubiri Jumamosi ijayo ya Aprili 20.

Je, Benchikha atabadili upepo wa mambo na kurejesha wimbi la ushindi Msimbazi au ataendelea pale alipoishia Roberto Oliveira ‘Robertinho’, aliyekumbana na kipigo cha aibu cha mabao 5-1 katika derby ya kwanza iliyopigwa Novemba 5 mwaka jana na kumfutisha kazi Msimbazi? Tusibiri tuone itakuwaje?

SOMA ZAIDI: Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc 

10 Comments

  1. Atulie tu kikosi cha simba ni kipana sana tatizo wanakosa muunganiko
    Kila mmoja anapambania jina lake binafsi na sio simba

  2. Kuondoka kwa benchika sio suluhisho la matatizo yanayoikabili Simba…ni wakati wa viongozi kukaa chini na kutafakari jinsi ya kuinusuru time yetu.

  3. Kuna wakati gari lenye dereva mzuri hupata ajali haina maana mara zote kuwa kosa ni la gari, barabara au dereva. Kuna wakati mifumo inakataana hivyo maboresho yanayotakiwa huwa makubwa itoke spea iwekwe nyingine, atoke mtu dhaifu awekwe Bora anaendana na mfumo. Kocha anao mfumo anahitaji watu wanao umudu, uondoke mfumo au spea!, kunyoa ama kusuka. Ni dhairi tairi ya gari mpya ni bora kuliko ya zamani ila tu isiwe feki.

Leave A Reply


Exit mobile version