Kocha mkuu mpya wa klabu ya Simba Abdelhak Benchikha ameelezea namna atakavyofanya kazi katika kikosi cha Simba ili kuhakikisha kuwa wekundu hao wa msimbazi wanapata mafanikio ndani nan je ya nchi.

Akizungumza wakati wa utambulisho wake kwa waandishi wa Habari, Benchika amesema kuwa anafahamu yanayoendelea lakini ana mikakati ya kuhakikisha Simba inafanya vizuri Zaidi. “Kuna mambo mengi ambayo tayari nayajua na nimekuja na mikakati ambayo nitaifanyia kazi. Kuhusu wachezaji tajua zaidi nikishaanza kazi, kuhusu mashindano ya ndani na kimataifa yote ni muhimu. Mimi ni mpambanaji na nitapambana hadi tutafika.”- Kocha mkuu Abdelhak Benchikha.

Aidha kuhusu kukubali kujiunga na wekundu wa msimbazi Benchika anasema alikua na shauku kubwa ya kujiunga “Nina furaha kubwa kuwepo hapa. Tangu nilipoanza kuwasiliana na viongozi nilikuwa na shauku ya kuja. Jambo kubwa ambalo naomba ni mashabiki kutupa ushirikiano na naamini kupitia hilo tutafanikiwa pamoja.”- Kocha mkuu Abdelhak Benchikha.

Lakini pia kuhusu wachezaji kocha huyo anasema kuwa hataangalia jina la mchezaji bali atapanga kikosi kutokana na kujituma kwa mchezaji mazoezini huku akiwataka mashabiki wa simba kuungana kwa Pamoja kuleta mafanikio klabuni “Mafanikio yatajengwa na Wanasimba wote hilo ndio muhimu zaidi. Kwa wachezaji sitaangalia majina bali anayefanya vizuri, kiwango cha mchezaji ndio kitafanya nimtumie.”

Leave A Reply


Exit mobile version