Kamanda

Bila shaka uko poa kabisa na unaendelea na maandalizi yako ya upambanaji hapo kwa Watoto wa mitaa ya Twiga na Jangwani yalipo makao makuu ya klabu ya Wananchi Yanga. Hii ni barua ya wazi kwako niliyoona nikuandikie baada ya kuona haya mengi yanayoendelea mitandaoni.

Nikiri wazi kuwa kwa kiwango cha beki wa kati kwa sasa, kama sio Ibrahim Bacca basi ni wewe kamanda Dickson Job kwa wachezaji wazawa na nisema kuwa ndio nakubali yupo Bakari Mwamnyeto lakini ni kama kiwango chake kimeshuka kiasi au amekosa kujiamini kuliko wewe.

Baada ya kuona kikosi cha Kocha wa Taifa Stars Hemedi Suleiman Morocco kama mwanamichezo nimeshtuka kuona jina lako halipo hapo yaani katika orodha ya wachezaji 23 watakaosafiri na Taifa Stars kwenda Azerbaijan jina lako Dickson Job halipo?

Imenipa maswali mengi haswa kutokana na kiwango chako ambacho unacho kwa sasa katika kikosi cha wananchi lakini naomba kukuuliza swali, hivi hizi tuhuma ni za kweli? Na kama ni kweli kwanini uliamua kufanya hivyo?

Binafsi mimi ni mtu wa mwisho kuamini kuwa ulikataa kucheza beki namba 2 jambo ambalo linaonekna kuwa ulidharau maamuzi ya kocha na kubwa zaidi wapo ambao wanasema kuwa umekosa uzalendo na taifa lako wewe unajiskiaje kwa sasa?

Kamanda, kama ni kweli basi tambua kuwa umeninyong’onyesha sana kwa kitendo hiki kwani hakika ile ilikua mechi yetu muhimu sana kwa Taifa. Kama si kweli basi tuendelee kuwapigia kelelee watu ambao wamekuwa wakifanya machaguo ya wachezaji wawe wanaangalia umuhimu na uhitaji kwenye kikosi cha Taifa Star siyo tu kuita wachezaji kwasababu una maslahi nao.

SOMA ZAIDI: Tuendelee Kuuamini Ukuta Wa Yerikho Simba SC?

 

Leave A Reply


Exit mobile version