Baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya CR Belouizdad kukamilika kwa wananchi kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza nilipokea simu kutoka kwa mdau wa Kijiweni ambaye mara nyingi huwa anafuatilia sana machapisho yetu katika tovuti yetu akipata taarifa hizi zaidi kutoka WhatsApp Channel ya Kijiweni.

Alinipigia simu na kusema kuwa ana barua yake ambayo anatamani iwafikie wengi haswa watu wa michezo kutoka hapa ndani nan je ya Tanzania nikamuambia anitumie ambapo baada ya kuituma nikaona niilete kwenu muisome na mniambie ujumbe umefika?

Barua yenyewe ilikuja ikiwa na kichwa cha habari “Simba imeridhika na kuhadaika na historia, Yanga ikiwa na kiu ya mafanikio na kutengeneza historia” na ikaanza kwa kusema,

 

Kwako Mhariri Kijiweni,

Kwanza hongereni timu ya wananchi.

Hakika mmeonyesha kile ambacho mashabiki zenu walikuwa wanakitegemea na kazi bora ya viongozi chini ya Rais wa klabu yenu Injinia Hersi Said.

Naomba niwaambie kuwa tofauti yenu na Simba kwasasa ni kubwa na hilo halina ubishi kabisa kwani mmekuwa ni timu ya kiushindani, kujituma, kujitoa, kucheza kitimu pamoja na nidhamu ya wachezaji.

Kwa miaka ya hivi karibuni mmeshaweka alama yenu kwenye mashindano ya Africa kuanzia kombe la shirikisho ambalo mlifika hadi hatua ya fainali na sasa mpo klabu bingwa mkitinga kwa kishindo hatua yar obo fainali  hakika mmeliheshimisha soka letu na mnauwezo wa kupambana na timu yoyote Afrika kwa ubora mlio nao sasa.

Sisi Simba bado tunaamini ni timu kubwa kwa nadharia ila kivitendo kwa sasa hamna kitu, wachezaji wazito kama hakuna kocha wa viungo, wavivu na wapo ambao ni wachoyo ambao wanatuonesha kuwa wanataka kujipambania rekodi zao na sio za klabu kwa ujumla.

Hongereni naona mkifika mbali kwa hali mliyokuwa nayo ya mafanikio. 

 

Bila shaka umeisoma na umeielewa barua hii ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kabisa na inayoeleweka. Maoni yako ni yapi? Unadhani kipi kinawafanya Yanga wanaendelea kutamba?

 

SOMA ZAIDI: Yanga Mmeniziba Mdomo, Mpira Ni Uwekezaji Sio Uchawi

Exit mobile version