Kwa heshima kubwa,
Natumaini barua hii inawafikia katika afya na ustawi mzuri wakati huu tunapoendelea na harakati zetu za kuinua kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania, ni muhimu kwa kila klabu kufanya maamuzi yanayofaa kuhusu njia wanazochagua kufuata kufikia mafanikio.
Napenda kutumia fursa hii kuwahimiza kila klabu kutathmini kwa makini na kuachana na imani za kishirikina katika michezo ambayo wanakuwa wanashiriki. Wakati imani hizi zinaweza kuonekana kama njia ya haraka ya kufikia mafanikio, ni muhimu kuelewa kuwa msingi wa mafanikio ya kweli unapatikana katika mazoezi ya bidii, nidhamu, na uwekezaji katika mafunzo ya kitaalamu na ndio maana kila klabu inakua na benchi la ufundi.
Imani za kishirikina zinaweza kuathiri sio tu maendeleo ya wachezaji binafsi lakini pia tasnia ya mpira kwa ujumla kwani kwa kujiingiza katika imani za kishirikina, tunaweza kudhoofisha uaminifu wetu katika mchezo, na hata kuwafanya wachezaji wetu kupoteza dira ya malengo yao ya muda mrefu wakiamini kwamba kuna nguvu za babu zitatumika kuwasaidia kushinda mchezo husika.
Badala ya kutegemea imani za kishirikina, nawasihi viongozi na wachezaji kuzingatia mambo muhimu kama vile:
- Uwekezaji katika miundombinu bora ya michezo na vifaa.
- Kuendeleza mipango ya mafunzo yenye tija na ya kisasa.
- Kukuza mazingira ya maadili na nidhamu katika kila ngazi ya mpira.
- Kujenga ushirikiano wa kujenga na kuimarisha mifumo ya klabu na ligi.
Kwa kufuata njia hizi, tutaweza kujenga msingi imara wa mafanikio ya mpira nchini Tanzania ambayo yanategemea uwezo halisi, jitihada, na maadili katika mchezo.
Tunaweza kufanikiwa tu tukifanya kazi kwa bidii na kuweka imani yetu katika misingi ya mchezo huu ambao tunauheshimu na tunautumaini. Natumaini mtazingatia wito huu na kuchukua hatua sahihi kwa faida ya mpira wetu na kizazi kijacho cha wachezaji.
Nawatakia kila la kheri katika juhudi zenu za kukuza mpira nchini Tanzania.
Kwa heshima kubwa,
Mhariri.
SOMA ZAIDI: Kwa Matukio Haya Bodi Ya Ligi Mjitafakari
3 Comments
Pingback: Azam vs Yanga Uchambuzi Na Takwimu Kabla Ya Mchezo - Kijiweni
Pingback: GUEDE Amemponza GAMONDI Kwenye Mfumo Wa Azam - Kijiweni
Pingback: Barua Kwako Pacome Zouzoua Profesa Wa Boli - Kijiweni