Hongereni kwa washambuliaji wote kwenye Ligi kuu ya NBC kwa msimu uliopita 2023/2024 moja kati ya msimu ambao ulikuwa mgumu sana kwenu, msimu uliyodhihirisha kuwa msimu mbaya sana kwenu washambuliaji wote na hilo halikwepeki kuwa ndani ya wafungaji bora 10 wa msimu ni washambuliaji wawili tu ambao ni Wazir Junior pamoja na Samson Mbangula walioingia.

Imetuchukua zaidi ya misimu 10 mfululizo bila kushuhudia jambo kama hilo kutokea, nikurejeshe nyuma kidogo hadi mwaka 2014 mpaka 2023 wafungaji bora walikuwa ni, 2014/2015 & 2015/2016 Amisi Tambwe (19) na (21), 2016/2017 Simon Msuva na Abraham Mussa (14), 2017/2018 Emmanuel Okwi (20), 2018/2019 Medie Kagere (23), 2019/2020 Medie Kagere (21), 2020/2021 John Bocco (16), 2021/2022 George Mpole (17), 2022/2023 Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza (17) pamoja na 2023/2024 ambapo mfungaji bora alikuwa Stephane Aziz Ki.

Takwimu zinaonyesha ndiyo msimu ambao ulikuwa mgumu na mbovu ambao ulikosa washambuliaji hatari zaidi kuliko misimu kumi nyuma ambayo mwisho wa Ligi Mfungaji bora alikuwa mshambuliaji.

Jambo ilo limenifanya niandike barua hii kwa washambuliaji wote kwa msimu ujao kuanzia Yanga SC iliyo na Prince Dube, Simba SC yenye Valentino Mashaka, Steven Mukwala na Fredy Michael, Azam FC yenye Jlacor Blanco, Singida Blacks Stars yenye Elvis Rupia, Joseph Guede na Habibu Kiyombo, Dodoma Jiji yenye Reliant Lusajo na Wazir Junior, Tanzania Prisons ambayo ina Samson Mbangula, JKT Tanzania ya John Bocco na Edward Songo, KMC FC yenye Ali Shabani pamoja na vilabu vingine vyote.

Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza, rejeeni tena misimu ya nyuma mjione namna ambavyo washambuliaji walidhihirisha ushiriki na uwepo wao kwenye Ligi kuu ya Tanzania kwa nyakati tofauti tokea ikiitwa Vodacom Premier League, Tanzania Premier League na sasa NBC Premier League.

Tarehe ya Kumbukumbu namba 2014/2015 hadi 2022/2023 inaelezea kuwa hakuna msimu ambao mfungaji bora wa msimu alikuwa ni kiungo na hata kwenye 5 hadi 10 bora basi orodha ilikuwa ikijaa majina ya washambuliaji wengi kuliko wachezaji wa nafasi nyingine, ni dhahiri kuwa kulikuwa na washambuliaji hatari ambao hawakuhitaji nafasi nyingi sana kufunga magoli bali wao walihitaji nafasi ya kucheza kupachika magoli ya aina tofauti tofauti.

Rejea msimu ambao ulikuwa na Obrey Chirwa, Medie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu, Prince Dube na wengine, magoli yao yalionyesha uchu wa kufunga na matumizi sahihi ya nafasi chache walizokuwa wakipata. Hakuna namna kwa msimu ujao kuhitaji washambuliaji bora wa kufumani nyavu kila mara na siyo wakaaji benchi.

Natumaini barua hii mmeisoma na kuipitia, ila naomba kuwajuza kuwa mpira umebadilika kiuchezaji ila siyo silaha ya kukosa washambuliaji wenye magoli mengi, uwanja wa mazoezi ndiyo sehemu ya kuonyesha uwezo wenu ila kwenye mechi ni mahala pa kuonyesha namna kazi yako unavyoifanya kiusahihi, nitarejea tena mwakani kukumbushia barua yangu ya 2024.

SOMA ZAIDI: Sio Vibaya Kuwaiga Simba Kwa Jambo Hili Ambalo Walilianzisha

5 Comments

  1. YAH, MAOMBI GA KUFUNGA MAGOLI YA KIKATIRII
    Ndg washambuliaji kwaheshima na tadhima SS mashabiki wa simba SC tunaomba mtulize akili zenu mjue tunawategemea sna na tumewapa Imani yetuu ko tunaomba mtulize MAGOLI ya viwango tukianza na utopolo tah 8

  2. Pingback: Udhaifu Na Ubora Wa Yanga Kwenye Mifumo Hii Kiwanjani

Leave A Reply


Exit mobile version