Mpendwa Pacome Zouzoua,

Natumai barua hii inakukuta ukiwa mzima japokua sijajua unaendeleaje na goti lililokufanya usimalize mchezo dhidi ya Azam Fc lakini natambua unapiga hatua kubwa katika kazi yako ya soka. Ningependa kwanza kabisa kukupongeza kwa juhudi zako zinazoendelea na mafanikio yako katika klabu ya Yanga. Umeonesha kiwango cha juu tangu ufike mpaka sasa kwani una uwezo wa kipekee na kujitolea kwako kwa timu.

Kutambuliwa kwa kiwango chako bora na kuitwa kujiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast ni hatua kubwa katika kazi yako ya mpira wa miguu japokua nafahamu kuwa ushawahi kuichezea kipindi flani. Hii ni heshima kubwa sana ambayo unastahili kupata. Kuwakilisha nchi yako katika viwango vya kimataifa ni ndoto ambayo wengi hunuia kuifikia, na wewe unapata fursa hiyo.

Hata hivyo, ninatambua pia umuhimu wa kuendelea kuihudumia Yanga kwani tunajua kuna michezo migumu mbeleni ambayo bila shaka ni muhimu mno kwa historia ya klabu ya Yanga pamoja na Tanzania kwa ujumla.

Hakuna anayepinga kwamba Yanga inakutegemea wewe Pacome na uwezo wako wa kipekee kuchangia katika mafanikio yao kimataifa kwani ushafanya maajabu makubwa mengi tu. Tunathamini mchango wako katika timu na jinsi unavyoleta uzoefu na ujuzi wako kwa wenzako.

Kwa hivyo, ninakuandikia barua hii ili kukuomba utafakari kwa makini chaguo lako. Unaweza kuendelea kuitumikia Yanga na kusaidia timu hii kufikia malengo yao waliyonayo, au unaweza kuchukua fursa ya kujiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast na kuiwakilisha nchi yako kwa Fahari ingawa tunafahamu mchezo wa mwisho ulipata majeraha na kushindwa kuumaliza mchezo.

Ninakuamini utafanya uamuzi sahihi kwa mustakabali wako binafsi na kazi yako ya mpira wa miguu. Tunakutakia kila la heri katika safari yako ya soka,

Kwa heshima na ukarimu,

SOMA ZAIDI: Barua Kwenu Washirikina Wa Mpira Wa Miguu Tanzania

2 Comments

  1. Pingback: Hili La AL HILAL Kucheza Ligi Kuu Ya Tanzania Limenitafakarisha - Kijiweni

  2. Pingback: Barua Kwa Waziri Ndumbaro Kuhusu Jezi Na Uzalendo - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version