Kwa heshima na taadhima nakuandikia barua mwamuzi Ahmed Arajiga,

Natumai barua hii inakukuta wewe na afya njema na ukiwa na ari kubwa zaidi kuelekea mchezo mkubwa wenye hisia kubwa zaidi miongoni mwa mashabiki unaozikutnisha klabu kubwa na kongwe Tanzania. Ningependa kueleza shukrani zangu kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukuamini na kupewa filimbi ya kuuhezesha mchezo huu.

Kama shabiki wa soka na mwanamichezo kutoka Kijiweni, tunatambua jukumu kubwa ulilonalo katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na uadilifu lakini pia natambua pia kwamba kazi yako ni ngumu na mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa.

Napenda kukusihi utumie uzoefu wako na hekima katika kusimamia mchezo huu. Tunakutia moyo kufanya maamuzi kwa kufuata sheria za mchezo bila upendeleo au kuweka taswira mbaya yoyote ile kwa wapenzi wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla ambao watakua wanaufuatilia mchezo huu. Tunaamini utaweza kusimamia mchezo kwa haki na kuepuka migogoro au utata wowote.

Sisi kama Kijiweni tunatambua kwamba jukumu lako ni muhimu sana katika kuhakikisha mchezo unamalizika kwa amani na furaha kwa pande zote mbili za mashabiki yaaani mashabiki wa Yanga lakini pia mashabiki wa Simba. Kwa hivyo, tunakuomba ufanye kazi yako kwa umakini na ustadi ili kutuletea matokeo yanayostahili.

Tunakutakia mafanikio katika mchezo wako na tunaamini kuwa utakua mchezo mzuri na wenye kuvutia zaidi kwa upande wako wa maamuzi lakini pia kwa mbinu za makocha pamoja na utekelezaji wa mbinu hizo na wachezaji kwa ujumla wao n ani wazi kuwa tnasubiri kuona mchezo mzuri na wa kuvutia.

Asante kwa kujitoa kwako na kwa huduma yako katika mchezo wa soka.

Kwa heshima kubwa,

Mhariri

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga

 

24 Comments

  1. Taisoni Chijoja on

    Kikubwa anatakiwa ajiamini na maamuzi anayo chukua ila asifuate mkumbo wa kele za mashabiki ataiharibu daby

  2. Nimuombe mwamzi asiwe Kama yule aliyeamua mechi ya yanga na mamelod aamuwe mchezo kwa haki na azingatie Sheria zote 17 bila upendeleo.

  3. Kevin Mbeikya on

    Pressure ni kubwa sana kuanzia kwa viongozi hadi wachezaji.
    Mwamuzi anabid kuhandle game vzr kulingana na ujuzi wake sio mapenzi binafsi.

  4. Mwamuzi akapambane ya ela yote asionee wala kuzulumu haki iwe sawa ili aepuke maneno ya watu kwa kaz yake

  5. beatusi ulalo on

    mimi nafikiri huyu refa yupo vinzuri kwani. kwanza ni mzoefu wa kuchezesha mechi kubwa hakika yangu ni mcheki mpira wa viwango vya juu kasimamie sheria na kanuni za mpira na mungu akutangurie

  6. Akazingatie sheria vizuri wala pessure ya wachezaji isi mtoe kweny mchezo mana izi game za derby wachezaj wanakua na pressure mpaka wanamtoa mwamuzi mchezoni

  7. Yeye ni refa mzuri sana
    Lakini kama ilivyo kwa waamuzi wetu hapa tz! Mahaba kwa timu zao hufanya wakose aibu na kuvuruga ladha ya mechi, ajitahidi tu kuwa thabiti…….. Hana baya arajiga

  8. Yeye ni refa mzuri sana
    Lakini kama ilivyo kwa waamuzi wetu hapa tz! Mahaba kwa timu zao hufanya wakose aibu na kuvuruga ladha ya mechi, ajitahidi tu kuwa thabiti…….. Hana baya Arajiga

    ILA IKIWEZEKANA AIBEBE TU SIMBA NISIWE MNAFIKI😂😂😂😂

  9. Pingback: Tabiri Sasa Matokeo Ya Dabi Ya Kariakoo Hapa Kijiweni - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version