Kwako Mo Dewji

Natumai barua hii inakufikia wewe na familia yako katika afya njema na ustawi wa kiroho na kimwili. Napenda kutumia fursa hii kuelezea mawazo yangu na kufikisha ombi muhimu kuhusu uwekezaji ndani ya klabu ya Simba.

Hakuna ambaye hafahamu kuwa Simba ni mojawapo ya klabu kubwa na ya kihistoria katika soka la Tanzania. Klabu hii imekuwa ikileta furaha na shauku kwa mamilioni ya mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hata hivyo, ili klabu iendelee kustawi na kufikia viwango vipya vya mafanikio, inahitaji uwekezaji mkubwa zaidi katika miundombinu, vifaa vya michezo, na maendeleo ya vijana.

Kupitia uzoefu wako na ujuzi wako katika uwekezaji, ningependa kuwasilisha ombi la kuzingatia uwekezaji ndani ya klabu ya Simba na wala sipingani na jinsi ambavyo umekua na mchango mkubwa katika mafanikio y klabu hii,lakini tambua kuwa uwekezaji mkubwa zaidi utasaidia kuboresha miundombinu imara na kuweza kuanzisha programu sahihi za maendeleo ya vijana, na kuimarisha kikosi cha Simba ili iweze kushindana kikamilifu katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Kwa ninayoyaona niwazi niseme kuwa mashabiki wamekosa imani kubwa kwa Try Again na Mangungu kwani wanaamini kuwa hawaujui mpira na fitina zake na ndio maana sasa hivi Simba imekuwa katika kipindi hiki cha kupata matokeo kwa shida. Na inaonekana kama vile watu wanaojua mpira Simba na wanaoweza fitina za mpira wakina Magori na Kaduguda japo bado wapo Simba lakini ni kama vile wamekaa pembeni wanatazama jahazi linavyozama. Hata Simba kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi mwaka huu ikiwa chini ya uongozi wa Try Again na Mangungu kwa kweli itakuwa ni bahati sana.

Mwisho kwa nini Try Again na Mangungu wasiwe waungwana tu wakajiuzulu ili waingie watu wengine wenye uwezo wa kuivusha Simba itoke hapo ilipo. Wanang’ang’ania nini kuongoza Simba wakati toka waingie kwenye uongozi Simba imepoteza makombe yote chini yao na hakuna dalili ya kupata hata moja msimu huu.

SOMA ZAIDI: Mashabiki SIMBA Wanahitaji Mabadiliko Makubwa Sio Propaganda

 

 

28 Comments

  1. Waondoke wte ad wachezaj walotuletea kina saido,boko, fredy,jobe tuletewe wachezaj wa maana simba ni tim kubwa sio ya kuwa na wachezaj wa viwango kam fred

  2. Endeleeni kushikana uchawi sisi yetu macho tarehe 20 msipokaa sawa 8 ili sisi tuwasimulie wanetu kizazi kijacho😂😂😂😂😂

    • Hao hawawezi jiuzuru kiwepesi zaidi ya wanachama na mashabiki kuwang’oa kilazima yaani watate wasitake ikiwezekana kipigo kiwepo tofauti na hapo hakuna kitu.

  3. Timu ya simba inabidi ifumuliwe ianzishwe na upwa na kusajili vyuma pia hao try again na kaduguda waondolewe ili kuijenga simba bora
    “SIMBA NGUVU MOJA💪💪💯💯”

  4. Toa Fredy,saido,jobe,kramo,babacar bila kusahau Baba ester shomy the way sarr Leta wa watu wa maana kina Fiston mayele ayoub aletewe msaidizi anaweza kumpa challenge msimu ujao tuta eshimiana tu

  5. Sasa me sielewi kwani mo ndo anatakiwa kuwachomoa hao jamaa au aende tu akawaambie
    Ila for sure simba saiv inaboa hatuwezi kuihama nyie hawajui mapenzi ya mpiraa wao wanatake easy tu sababu wao wanapata wanachotaka ila mashabiki hatupati haki yenu ya kuona timu yetu inafanya vizurii

  6. Kiukweli try again na mangungu na imani kajula wangependwa na Simba milele kama watajiuzulu wenyewe kuliko kung’ang’ania uongozi ambao hawauwezii….

  7. Me naomba wangalie kama tatizo lipo kwa viongoz na baadh ya wachezaji Raisi wa simba awatoe tunaumia sana na tunapoteza matumaini kwa timu yetu tunaumia 😭

  8. shida huwenda sio wachezaji ,kwani timu walizotoka si waliwaka il mbona baada ya kuja tu uku viwango vyao vimeshuka , Cha msingi ni kuangalia kwanini wakija simba hawachezi Kam uko waliko Toka. SHIDA n nini haswa

  9. Sir. Walter Winstone on

    Listen very careful and with all the attention, Simba imeacha kuwa football club imeanza kua business club, why? Hatukatai kila club ina nyakati za kupanda na kushuka hata vilabu vikubwa duniani tunaona.. kwa upande wa Simba sio kwamba tunashuka kwasababu ya nyakati hapana Bali ni sababu baadhi ya watu wamefanya club kuwa chanzo Cha mapato.. wachezaji na team husika wameacha ku focus na mpira wanawaza biashara.. mchezaji hawezi waza kufanya mazoezi na matangazo ya wadhamini wao at the same time hiyo ni point no 1. (Kwanini wasiajiriwe watu special kwa ajili hiyo?. Point no 2. Uuzaji na ununuaji wa wachezaji, kumekuwa na wimbi la kiswahili la ununuaji wa wachezaji ili ku washtua wapinzani kua sisi ni Bora sana na tuna Hela badala ya kuchukua wachezaji wenye ubora na kuruhusu wachezaji hao kupata nafasi ya kuonyesha walichonacho kwa wakati sahihi.. swali, naomba ufafanuzi wa Moses phiri kwanzia usaliji wake, malengo yake kabla ya kuja Simba, kwa kiwango gani ameitumikia Simba na muhimu zaidi aliemuona Moses phiri hadi akamsajili ni nani na kwanini aliuzwa. Point 3. Ununuaji wa makocha. Tumeona uongozi mwingi sana na tumekua mashahidi wa matokeo ya coaches hao, Simba ni club ya Tanzania uzalendo kwanza, tuliona uongozi wa Juma Mgunda kama head coach simba ambapo timu ilikua katika kiwango kizuri mmno, ufungaji, chemistry, accuracy, fitness, good communication skills among leaders na wachezaji.. swali, kwanini Juma Mgunda hakuaminika apewe head coach aendelee na strategies zake kuisogeza Simba mbele? Kwanini tumekua walimbukeni na raia wa kigeni?
    Okay tumempata benchika ameikuta Simba Iko hoi na kaikuta nusu msimu, angalia Benchika ni kocha, ana strategies zake.. anajaribu kutengeneza kikosi kwa njia zake mwenyewe.. ambacho anajua ni kua Simba Iko builded tayari na ina watu specific ndo mana anajaribu kutu prove wrong na kila akijaribu matokeo ni -ve( kinamkost).
    Cha msingi Tuupe muda wakati usogee.. tufikiri kabla ya kutenda.. Simba ina kikakitu kinachotuponza ni pressure kutoka nnje.. tunaweza tusisajili yeyote na tukachukua ubingwa wa African inshallah, ebu tujitafakari alafu.
    1.Tusafishe magugu yote bila kujali tutaonekanaje.
    2.Tuache biashara kwanza tufanye mpira.
    3.Tuwe wavumilivu wa nyakati kwa kutumia akili.
    UJUMBE
    Kila kitu kizuri ni matokeo ya kitu kibaya. Let’s think before doing anything.

  10. mm naomba club ya simba kupitia management yake,,ivunje kabisaa utawala uliopo madarakani kwa sasa na kuleta viongozi mahiri ambao wataweza kuifikisha club panapotakiwa na ndio kiu yetu mashabiki zaidi ya hapo tutakuwa uvumilivu in short

  11. Pingback: Ligi Kuu Bara Iko Kwenye Vita Ya Mfungaji Bora Kiungo - Kijiweni

  12. Pingback: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version