Natumai barua hii inakukuta ukiwa mzima na mwenye afya njema kabisa Feitoto. Napenda kukupongeza kwa ujasiri wako na maamuzi magumu uliyowahi kuchukua ambayo mpaka sasa naweza kusema bado yaliacha vidonda kwa baadhi ya mashabiki wako. Inaeleweka kuwa maisha ya mpira wa miguu yanaweza kuwa na changamoto nyingi, lakini uamuzi wako yalionesha ukomavu na uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wako.

Mimi kama shabiki wako naamini kuwa kila hatua unayochukua katika kazi yako ina umuhimu wake, na naweza kutambua juhudi zako na mchango wako kwa klabu yako ya Azam FC. Kuwa na ujasiri wa kufuata njia yako mwenyewe ni jambo la kuthamini, na naamini utaendelea kuonyesha uwezo wako uliokithiri.

Achan ana haya yanayoendelea mtandaoni kukuhusu kwamba haukua na baraka kutoka kwa mashabiki wa mitaa ya Twiga na Jangwani kutokana na jinsi ulivyoondoka katika klabu hiyo na jinsi ambavyo mafanikio waliyoyapata baaada ya kuondoka kwako, lakini pia na kelele zilivyokuwa nyingi mpaka usajili wako ndani ya Azam Fc.

Niko nyuma yako Feitoto kama shabiki wako lakini kumbuka kuwa siku zote mheshimu mkubwa wako hata ukiwa umemzidi utajiri kiasi gani usijrudia tena ile kauli ya kuwa huyu na yule mara hivi na vilena na nakutakia mafanikio makubwa katika safari yako. Tunategemea kuona mafanikio yako uwanjani na kwa kila jambo jipya unalolenga kufanya. Endelea kuwa na bidii, kujituma, na kuwa mfano kwa wachezaji wenzako.

Natatarajia kukuona ukiendelea kung’ara na kufanikiwa katika kila hatua ya maisha yako ya mpira wa miguu.

 

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga

Leave A Reply


Exit mobile version