Kwa wachezaji wa Simba,

Natumaini kwamba barua hii inawapata nyote katika hali njema na hamu kubwa ya kuelekea kwenye mchezo muhimu wa robo fainali dhidi ya Al Ahly huko Misri. Ni mchezo mkubwa lakini naamini kuwa kama ilivyo Nguvu Moja basi kwa pamoja na umoja wenu bila kusahau juhudi zenu Simba inakwenda kufuzu hatua ya nusu fainali na kufikia mafanikio makubwa.

Mchezo huu ni fursa ya kipekee ya kuthibitisha uwezo wenu kama timu bora kutoka Afrika Mashariki na Kati.Ni nafasi ya kipekee ya kuonyesha ulimwengu wa soka uwezo wenu na kutimiza ndoto za mamilioni ya mashabiki wenu wanaowasapoti kwa moyo wote.

Nina imani kubwa katika kila mmoja wenu.Najua kuwa Al Ahly ni timu ngumu na yenye uzoefu mkubwa, lakini hilo halipaswi kuwafanya muogope au kupunguza juhudi zenu. Badala yake, ni wito kwnuu kufanya kazi kwa bidii zaidi, kutumia kila uwezo wenu, na kucheza kwa moyo wote.

Kila mmoja wenu ana jukumu muhimu katika kufanikisha malengo ya klabu ya Simba.Mnahitaji kujituma kila dakika ya mchezo, kuwa na nidhamu ya hali ya juu, na kufanya maamuzi sahihi kila wakati. Mnapojitolea kwa pamoja na kucheza kama timu moja ni rahisi kufikia mafanikio makubwa.

Maandalizi ni muhimu sana. Kila mmoja wenu anahitaji kujiandaa kikamilifu kimwili na kiakili. Mnahitaji kuwa na imani na ujasiri katika uwezo wenu wenyewe na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha mnakuwa tayari kwa kila kitu.

Napenda kuwasihi mjisikie fahari kuvaa jezi ya klabu ya Simba na kuiwakilisha kimataifa kwani hii ni fursa ya kipekee ya kufanya historia na kuandika jina lenu katika soka la Afrika. Ni wakati wenu wa kung’aa na kufikia mafanikio makubwa.

Msikate tamaa, msikubali kushindwa na naamini kuwa mkicheza kwa moyo wote na kufanya kazi kama timu moja, hatuna shaka kuwa mnaenda kufikia mafanikio makubwa.

Kama ilivyo nguvu moja basi kwa umoja na ujasiri ni wakati wa kuonesha maana halisi ya neno Nguvu Moja nchini Misri na ninawatakia kila la heri katika maandalizi yenu

Iwakilisheni Simba kwa heshima na ujasiri, na kwa pamoja mtashinda.

Kwa heshima kubwa,

Mhariri

SOMA ZAIDI: Barua Hii Iwafikie Wachezaji Wa Yanga Huko Afrika Kusini

4 Comments

  1. Mungu afanye muujiza kama siku ya mkate mmoja na samaki wawili wakala maelef ya watu na wakasaza ndivyo navoiombea Timu yangu ‘ msiogope mjiamini tuko nyuma yenu tunawaamini msituangushe plz

  2. Ata mie pia naongezea kwa kusema simba ni timu kubwa nasyo mara ya kwanza kucheza nahao wamisri khyo mnatakiwa kujiamini na kucheza kwa malengo yakuingia nusu fainali ninaiman na benchi la ufundi pamoja na wachezaji pia nawaombea kwa mwenyezi Mungu awajaze nguvu afya njema ili muweze kufanya vizuri nakupata ushindi mkiwa ugenini

Leave A Reply


Exit mobile version