Kwako Barbara Gonzalenz,

Natumai umzima wa afya kabisa na unaendelea na majukumu yako mengine kama kawaida Barbra lakini pia natumai unaendelea kuifuatili vyema klabu yako ya Simba ambayo bila shaka kamwe huwezi kuacha kuifuatilia.

Mimi ni moja kati ya mtu ambaye si shabiki wa Simba lakini nilikua mpenzi wa namna ambavyo ulikua ukifanya majukumu yako katika klabu ya Simba kama Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hii kubwa yenye historia kubwa ya soka katika nchi ya Tanzania lakini pia na Afrika Mashariki na kati.

Naweza kusema ilikua ndio mara yangu ya kwanza kabisa kuona mtendaji mkubwa wa maamuzi ndani ya soka tena katika klabu kubwa akiwa ni mwanamke ni wazi kuwa aliekuamini na kukuweka pale alikuona ukiwa na ndoto kubwa ya kutaka mafanikio ya Simba na yalipatikana.

Ni wazi nakumbuka maamuzi yako ya kishujaa pale inapotokea jambo ambalo linahitaji maamuzi lakini pia bila kusahau kuwafanya mashabiki kuwa na Imani zaidi na klabu yao bila kusahau kwenye kuhakikisha kuwa wanakua wanajitokeza katika kupambania klabu yao.

Najua wapo ambao walikua hawakupendi kwa sababu zao wanazozijua wao kuanzia ndani ya timu mpaka nje ya timu lakini najua tupo ambao tunakupenda na tulikupenda lakini bado tunatamani kukuona ukirejea katika majukumu yako ya kila siku katika kupambania klabu ya Simba.

Nikiri kuwa licha ya kwamba yupo mtendaji mkuu mwingine lakini bado naona kama Simba inahitaji uwepo wako ndani ya uongozi ili kuhakikisha kuwa itikadi ngumu na zenye manufaa kwa klabu ya Simba zinatekelezeka kwa haraka lakini pia na kuedelea kuipambania nembo ya simu.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Mwanamichezo

SOMA ZAIDI: Fredy Anahitaji Msaikolojia, Ana Tatizo Hili Kubwa

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Klabu Zilizowahi Kushinda Mataji Ya Ligi Kuu Tanzania Bara - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version