Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON nchini Ivory Coast tayari vikosi vitakavyowakilisha nchi zilizofuzu vimekwishatangazwa na moja ya kikosi kilichotangazwa ni cha timu ya Taifa ya Mauritania kikiwa na golikipa mrefu zaidi katika michuano hii anayefahamika kama Babacar Diop Niasse.

Babacar ni golikipa anayechezea kikosi cha FC Nouadhibou kinachopatikana nchini Mauritania na amezaliwa katika jiji la Ksar nchini Mauritania tarehe 17/09/1995 akiwa na urefu wa Mita 1.90 na futi 6 na inchi 3 anatajwa kama golikipa mrefu zaidi katika michuano hii ya AFCON 2023.

Licha ya kuchezea klabu ya FC Nouadhibou lakini pia aliwahi kuchezea timu kama ACS Ksar ya kwao ambapo alicheza msimu wa 2016 hadi 2018 kabla ya kutimkia katika kikosi cha ASC Police kuanzia msimu wa 2018 mpaka 2021 kabla ya kujiunga na Nouadhibou anayochezea mpaka sasa.

Wakiwa na kocha Amir Abdou, Mauritania au jina lao la utani kama Mourabitouns wamefuzu Afcon msimu huu kwa kupata ushindi dhidi ya Sudan wa mabao 3-0 huku wakisare mchezo wa kwanza dhidi ya Gabon kwa bila ya kufungana lakini pia wakipoteza mara 2 mbele ya DR Congo na kushinda mechi 2 za mwisho ambapo alimfunga Sudan bao 3:0 na Gabon bao 2:1.

Hawajawahi kuchukua ubingwa wa AFCON lakini hii ni mara yao ya 3 kushiriki katika michuano hii ya AFCON ambapo katika ngazi ya dunia wanashika nafasi ya 105 na hii kwa mujibu wa takwimu za FIFA na wamefuzu AFCON wakitoka kundi I.

Golikipa huyu ana kibarua Kizito cha kuhakikisha nyavu zake hazitikswi na wapinzani kwani wamepangwa kundi D akiwa na timu kama Algeria, Angola na Burkina Faso zenye wachezaji wenye uchu wa kuweka rekodi katika michuano hii kwa msimu huu. Michuano ya AFCON inatarajiwa kutimua vumbi kuanzia tarehe 13/01/2024 mpaka tarehe 13/02/2024 nchini Ivory Coast

Endelea kufuatilia zaidi taarifa mbalimbali kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.

 

 

 

 

 

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Makocha 5 Wanaolipwa Pesa Ndefu Zaidi AFCON - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version