Uwanja wa Baba Yara ni uwanja mkubwa wa mpira wa miguu uliopo Kumasi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana. Uwanja huo uko katika eneo la Racecourse, ambalo ni kitovu cha shughuli za michezo Kumasi. Uwanja wa Baba Yara ulijengwa mwaka 1959 na ukafunguliwa rasmi mwaka 1959. Jina lake linatokana na kumuenzi Baba Yara, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa Afrika wakati huo.

 

Uwanja huo una uwezo wa kuchukua karibu watazamaji 40,000. Urefu wa uwanja huo ni mita 110 na upana ni mita 75. Uwanja wa Baba Yara unapokea mechi za ligi kuu ya Ghana, mechi za timu ya taifa ya Ghana na pia mechi za kimataifa kwani umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unajivunia vifaa bora vya michezo kama vile nyasi bandia, taa za kisasa na vifaa vingine muhimu kwa michezo. Pia una vyumba vya kubadilishia nguo na vyoo vya kisasa kwa ajili ya wachezaji na mashabiki.

Huu ndio muonekano wa uwanja wa Baba Yara wa nchini Ghana.

 

Asante Kotoko ni moja ya timu kubwa na maarufu nchini Ghana ambayo uwanja huu wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani kwa mechi zao za ligi kuu lakini pia na zile za kimataifa. Pia umewahi kuandaa mechi za mashindano makubwa kama vile Kombe la Mataifa ya Afrika na michezo ya Jumuiya ya Madola ni sehemu muhimu ya historia ya michezo nchini Ghana na unachangia katika ukuaji na maendeleo ya soka nchini humo.

Uwanja wa Baba Yara uliopo Ghana unatumika na timu ya mpira wa miguu ya Asante Kotoko Sporting Club, ambayo ni moja ya timu kubwa na maarufu nchini Ghana. Uwanja huo pia hutumiwa na timu nyingine za ligi kuu nchini Ghana pamoja na timu za kitaifa za Ghana.

Hii ndio historia ya uwanja huu mkubwa zaidi nchini Ghana uliobeba historia mbalimbali ambao Wananchi watakipiga dhidi ya Medeama majira ya saa 1 za jioni. Soma zaidi kuhusu Medeama hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version