Ni miezi kadhaa sasa imepita tokea Ligi kuu ya NBC kutamatika na kumjua bingwa mpya wa Ligi hiyo ambae ni  klabu ya Yanga namna walivyokuwa wanacheza ilionyesha dhahiri ubora wa kikosi chao na muunganiko wao.

Kikosi kilichokuwa kinaanza kilikuwa na muunganiko huku kukiwa na wachezaji tegemeo zaidi kikosini na kuna wakati baadhi yao walikuqa hata wakikosekana bado timu ilikuwa inapata ushindi lakini pia kuna ambao walikuwa wakikosekana basi tofauti kikosini inaonekana jambo ambalo kwa kiasi fulani ilikuwa inakiadhiri kikosi hicho japo siyo kwa kiasi kikubwa kwanini ?

Timu ilitengenezwa kutegemea na siyo kumtegemea mtu mmoja tu jambo ambalo lilimpa nafasi kubwa kocha mkuu kutengeneza imani kwa kila mchezaji kuweza kuamini kuwa akipata nafasi anatakiwa kuonyesha kile alichonacho na kumpa imani Kocha ya kumuamini na kumpa nafasi zaidi.

Licha ya kuwa na kikosi chenye muunganiko lakini kuna mapungufu kadhaa yalikuwa yakionekana kwenye baadhi ya maeneo kikosini na eneo mama zaidi lilikuwa eneo la mwisho la upachikaji mabao (eneo la ushambuliaji) na nafasi aliyokuwa nacheza Khalid Aucho kukosekana kwake kulikuwa kunasababisha namna ya uchezaji kikosini kubadilika, sasa maboresho yamefanyika ?

Kwa kiasi kikubwa usajili wa msimu mpya wa Ligi uligusa maeneo mama ambayo yalikuwa yanaonekana zaidi yana mapungufu au yalihitaji maboresho zaidi.

Moja, ni ushambuliaji, msimu uliyopita eneo ilo halikuwa bora sana na  kupelekea eneo ilo kufunga magoli machache licha ya kuwa ndiyo kazi rasmi ila haikutekelezwa ipasavyo na kupelekea wafungaji kuwa ni viungo kuliko washambuliaji.

Sasa usajili huu uligusa eneo ilo kama wengi walivyotarajia na kuwasajili Prince Dube ambaye hakuna mtu ambaye ana shaka na ubora wake kwenye eneo la mwisho la kupachika mabao pamoja na Jean Baleke ambaye pia hakuna mpenzi wa soka na mfuatiliaji atakataa kuwa ana “Quality” nzuri sana ya kufunga na kuwa sehemu ya timu bora kama Yanga SC, usajili wa wachezaji huo unafaonyesha kuwa kuna asilimia kubwa maboresho ya eneo ilo yakawa makubwa tofauti na msimu uliyopita.

Pili, eneo la kiungo mkabaji, kuongezwa kwa kiungo Aziz Andambwile kama kiungo mkabaji kuja kusaidiana na wengine kikosini, uchezaji wa Andambwile kwa kiasi kikubwa utasaidia sana kikosi hicho kuelekea msimu mpya wa mashindano na kumpa nafasi kubwa Kocha ya kumtumia kiungo mwingine au hata akikosekana  Khalid Aucho basi anaweza kumtumia Andambwile.

Tatu, ni eneo la kiungo mshambuliaji, moja ya eneo ambalo Yanga SC walikuwa bora zaidi msimu uliyoisha ni eneo ilo uwepo wa viungo Aziz Ki, Max Nzengeli, Pacome Zouzoua, Sure boy iliifanya kuwa moja ya safu bora kwenye Ligi na kikosi icho.

Lakini nje ya uwepo wa wachezaji hao ila maboresho au nyongeza ya wachezaji wengine kikosini ni dhahiri kuna ongeza upana wa kikosi hicho na matumizi makubwa ya mifumo mbalimbali, uwepo wa Clatous Chama utampa Kocha nafasi nyingine kimfumo na kimbinu kuweza kumtumia mchezaji huyo ambaye hakuna mtu hasiyejua ubora wa kiungo huyo.

Pia usajili wa kiungo Duke Abuya nao ni bora kwa kikosi hicho ubora wa Duke Abuya utaongeza kitu kwani nje ya kuwa kama kiungo mshambuliaji lakini kati ya wote yeye ni moja ya kiungo ambaye anaweza kutumika kusaidia kukaba na akafanya vyema na pale atakapohitajika kushambulia akafanya pia kwa usahihi, ni moja ya usajili nzuri sana kwenye dirisha ili ndani ya kikosi cha kocha Miguel Gamondi.

Kikosi cha Yanga SC hakina maboresho makubwa sana na hiyo imejidhihirisha kwenye mchezo wa kirafiki utofauti wa Yanga SC ya msimu uliyopita na ya msimu ujao ni ndogo sana na moja ya maboresho yao ni kuwa na upana wa kikosi unaompa kocha Gamondi nafasi kubwa ya kubadilika kimbinu na kimfumo pia.

Moja ya eneo ambalo nililiona likiwa na maboresho ni kukimbia eneo kubwa la uwanja wachezaji walikuwa wakikimbia eneo kubwa la uwanja kwa muda wote wa mchezo jambo ambalo linadhihirisha ubora wa utimamu wa mwili “Fitness” kwa wachezaji wa timu hiyo.

Matarajio, msimu uliyopita ubora wao ulikuwa kwenye “Fitness” kitu ambacho pia kwa msimu ujao ndiyo itakuwa silaha yao kubwa sana, wakati ambao timu nyingi zinakuwa chini hususa muda wa mchezo unapoelekea ukingoni basi Yanga SC walikuwa bora sana na ilo nalitarajia kuliona kwa msimu ujao 2024/2025.

SOMA ZAIDI: Fadlu Davis Na Mtihani Mzito Wa Uvumilivu Na Imani Simba

2 Comments

  1. Pingback: Ligi Kuu Inakaribia Hivi Ndivyo Wazawa Wanatakiwa Kufanya

Leave A Reply


Exit mobile version