Ni Azam dhidi ya Yanga, Moja ya mchezo mkubwa na wenye kuteka hisia za wapenda mpira nchini na hiyo inatokana na mchezo huo kuwa na msisimko mkubwa timu hizo zinapokutana hususani ndani ya Dimba la Benjamini Mkapa, kasi ufundi magoli na huokoaji wa hatari kwa magolikipa.

Mpaka sasa kwenye michezo yao mitano Ya mwisho waliyokutana kikosi cha Yanga SC kimefanikiwa kuibuka na ushindi michezo 4 na kutoa Sare moja jambo ambalo ni kuwa Azam FC imeambulia alama moja pekee ndani Ya michezo 5 dhidi Ya Yanga SC.

Hata hivyo ushindi wa Yanga SC dhidi ya Azam FC huwa unakuwa ni watofauti Ya goli moja pekee, kuanzia msimu wa 2021/2022 Yanga SC amefunga jumla ya magoli 12 na kuruhusu saba huku Azam FC akifunga magoli 7 tu na kuruhusu 12. Kinara wa ufungaji magoli ndani Ya michezo yao 5 ya mwisho ni Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Stephane Aziz Ki ambaye amefunga jumla Ya magoli 4 ambaye ana nafasi ya kuongeza magoli yake kwani bado ni sehemu ya Kikosi cha Yanga SC akifatiwa na Fiston Mayele ambaye hayupo mwenye 3 na wa tatu ni Feisal Salum mwenye magoli 2 (sasa yuko Azam FC).

Takwimu zinaonyesha kuwa timu hizo zilipokutana kwenye michezo yao mitatu ya mwisho magoli mengi yamefungwa kipindi cha pili kwani yamefungwa jumla ya magoli 8 na magoli 6 yamefungwa kipindi cha kwanza ishara ambayo inaonyesha kuwa wanafungana sana kwenye kipindi chochote cha mchezo hivyo kwenye mchezo wao lazima wafungane.

Msimu huu mpaka sasa Yanga SC yuko kileleni kwa alama nane na mpaka wanakutana Azam ana alama 44 nafasi Ya tatu na Yanga SC ana alama 52 nafasi Ya kwanza, ndani Ya michezo yao mitano Ya mwisho kwenye Ligi kuu msimu huu Yanga SC amefanikiwa kushinda michezo yote na kukusanya alama 15 huku akifunga magoli 14 na akiruhusu magoli 2 tu, kwa upande wa Azam FC kwenye michezo yao mitano Ya mwisho kwenye Ligi kuu ya NBC wamekusanya alama 9 wakifunga magoli 7 na wakiruhusu magoli 3 tu.

Kinara wa upachikaji mabao kwa Yanga Sc ni Aziz Ki mwenye magoli 13 akifatiwa na Max Nzengeli mwenye magoli 9 na upande wa Azam FC kinara akiwa ni Feisal Salum mwenye magoli 12, huku Kipre Junior akiwa kinara wa kutengeneza magoli “Assist” kwa pande zote mbili akifanya hivyo mara 8 akifatiwa na Yao Attohoula mwenye 7, Stephane Aziz Ki mwenye 6 pamoja na Feisal Salum mwenye “Assist” tanò.

Azam FC wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-3-3 pamoja na 4-4-2 ambapo silaha yao kubwa ni kutokea pembeni kwani wana wachezaji wenye kasi mwendo na skills kufanya hiyo kwa usahihi Kipre Junior, Gibril Sillah, Ayoub Lyanga pamoja na Iddy Nado. Mara nyingi huwa wanautumia Feisal Salum kama namba 10 na huwa anafahidika na nafasi hiyo akikaa nyuma ya mshambuliaji na mipira ya pili inayookolewa anakutana nayo, uwepo wa kinda Pascal Msindo imekuwa silaha yao upande wa kushoto akiwa anapanda kusaidia mashambulizi na kushuka kukaba kwa wakati na usahihi.

Wamekuwa wanacheza vizuri wanatengeneza nafasi na kufunga pia ila changamoto yao kubwa kwa sasa ni kuruhusu magoli kwanini? Wanakuwa wanaacha mianya sana hususa eneo lao la kati na kuwapa wapinzani nafasi ya kulifikia goli lao kwa urahisi, Nini wafanye kuboresha ilo kwenye mchezo huu ? Moja ni kukabia chini kuifanya timu kuwa “compact” sana na kukimbia sana na zaidi kutumia “Caunter attack” kutokana na kuwa na wachezaji ambao wana kasi kitakachobaki ni usahihi wa kutumia nafasi watakazotengeneza.

Kwa upande wa Yanga SC wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-2-3-1 jambo ambalo wanaufanya mchezo kuutawala zaidi eneo la kati wakiwa na Viungo wawili wenye asili ya kukaba na watatu washambuliaji huku wakiwa wanatokea katikati zaidi na ubadilika na kutokea pembeni pia, ipi silaha yao kubwa? Moja ni kuwa na uhakika wa kufanya “Press” kwa mpinzani wao muda wote wa mchezo wakianzia juu kwa mshambuliaji wao na mara nyingi Clement Mzize na Kennedy Musonda wamekuwa wakifanya kwa usahihi kuwapa presha mabeki wa upinzani, pili ni ufanisi na pasi za hatari za Aziz Ki ndiyo Mchezaji anayecheza kwa uhuru zaidi kikosini akizunguka eneo kubwa la uwanja pamoja na uwezo wake wa kupiga mashuti.

Kipi wafanye kuwashinda Azam ? Kubwa zaidi ni kuendelea na namna yao wanayofanya “press” Kwa mpinzani na itakuwa vizuri wakianza na Clement Mzize au Kennedy Musonda kama namba 9 na pili ni kupitia katikati mwa uwanja eneo ambalo kwa sasa Azam FC wanapitika kirahisi zaidi.

Zaidi ni kuwa tutarajie mchezo mzuri wenye kasi na ufundi ndani yake na hiyo inatokana na timu zote mbili kuwa na wachezaji wenye uwezo, kasi na ufundi kutokea pembeni na katikati mwa uwanja pia, kikubwa ni kuwa kuna nafasi kubwa kwa timu zote kupata goli huku wachezaji wa kuchungwa zaidi wakiwa ni Aziz Ki, Feisal Salum, Kipre Junior pamoja na Max Nzengeli.

SOMA ZAIDI: Barua Kwenu Washirikina Wa Mpira Wa Miguu Tanzania

Leave A Reply


Exit mobile version