Yanga katika msimu wao bora wa 2023 / 2024 hakuna timu iliyowapa changamoto kama klabu ya Azam hii ni kutokana na uwezo mzuri wa wachezaji wa azam mbinu za mwalimu Dabo ambazo zimekuwa zikimpa changamoto kocha wa Yanga Gamondi

Kabla ya kuangazia mchezo wa leo tuangalie kwanini azam huwa wanampa changamoto yanga katika michezo waliyokutana chini ya mwalimu Dabo . Baada ya mwalimu wa Azam kujua kuwa wachezaji wengi wa timu yake ni wachezaji wenye uwezo wakiwa na mpira mguuni kuliko wakiwa wanaukimbiza mpira akaamua kuwa muumini wa mpira wa kusogea mbele kwa kutumia pasi kuliko mipira mirefu

Staili hii inawafanya wacheze kwa kasi na kubadilishana nafasi sana kitu ambacho ni changamoto ukitaka kuwakaba katika mstari wa katikati (midblock) na hiki ndicho yanga wamekuwa wakifanya dhidi yao ambacho kilikuwa faida kwa azam katika nyakati kadhaa

Katika mchezo wa leo wa fainali ya CRDB Federation cup utakuwa ni mchezo wa kimbinu ambao pia utategemea uwezo wa mchezaji mmona mmoja mara nyingi azam akicheza na yanga amependa kutoka nyuma ya mpira katika umbo la wachezaji watatu (mabeki wakati wawili na beki mmoja wa pembeni ) huku yanga wakiwa na wachezaji wawili wakuweka pressure kwenye mpira na kutengeneza umbo la 4-4-2 hivo ni 3-5-2 azam wakiwa na mpira na 4-4-2 yanga wakiwa hawana mpira

Hii ndivyo inavotokea mda mwingi wakikutana japo haiweki uwakika kuwa leo itakuwa hivi pia

Yanga wamekuwa wakipenda kuacha idadi kubwa ya wachezaji kwenye boksi lao endapo wanakutana na mpinzani ambaye wanashaka na uwezo binafsi wa wachezaji wa timu hiyo lakini kwa kawaida yanga wamekuwa wakicheza katika mfumo wa 4-2-3-1 ambao umekuwa ukinyumbulika mda ambao wanajaribu kusogeza mpira mbele aidha kuwa (3-4-3) (4-3-3) pia .

Azam wana madhaifu yakumkosa mtu mwenye uwezo wa kubeba mpira kwenda mbele (ball progressor) hii inaweza ikawa na faida katika kuwavutia wachezaji wa timu pinzani kwenda kuweka presha na kuacha nafasi nyuma yao ambayo inaweza kutumika na washambuliaji wao kitu kinachowalazimu wausogeze mpira kwa kutumia pasi nyingi na kubadilishana nafasi kwa wachezaji.

Kwa upande wa yanga silaha yao kubwa imekuwa namna Gamondi anavowatumia (pacome , max , aziz ki ) Faida anayopewa na hawa watu watatu imemfanya awe na idadi kubwa ya nafasi zinazotengenezwa kwasababu ya uwezo wao wa kusogeza mpira mbele na kutengeneza nafasi nyingi pia wakisaidiana na Yao pamoja na kibabage au lomalisa kama mabeki wa pembeni

Timu zote mbili zina faida ya wachezaji wenye uwezo mkubwa (bangala , akamiko , feisal , akamiko ) hawa wote ni wazoefu na wenye uwezo kwa yanga pia (Aziz ki , Max , Pacome , Guede ) wanauwezo wa kuamua mchezo kwa uwezo wao binafsi endapo mbinu za walimu wao zitaenda mlama

Gamondi ana nafasi yakujiuliza mchezo wa mwisho alizidiwa wapi na  Dabo anajua alifaulu wapi na aongeze nini ili aweza kumiliki na kudhibiti yanga na viungo wao wasitengeneze nafasi nyingi.

SOMA ZAIDI: Uso Wa Saido Ntibazonkiza Unazungumza Mengi

9 Comments

  1. Pingback: Wachambuzi Wanamuingiza Feitoto Kwenye Chuki

Leave A Reply


Exit mobile version