Matumizi ya Nafasi yameamua Dakika 90 za Kasi na Ufundi kwa Timu zote mbili. Azam wakitumia zaidi pembeni huku Simba wakitumia Katikati na upande wa kushoto zaidi

2-3-2-3 ya Azam FC in Build-up(Fuentes & Bangala as CBs then Zaydi, Akaminko + Chilambo/Msindo lakini pia wanabadilishana kucheza as AM na Fei Toto mwisho Syllah, Kipre + Iddi Nado ambao waliunda mstari wa watu wanne pia Azam ilipocheza 2+3+1+4)! Wapi walipata ugumu?

  1. Kuzuia MH15 & Mwenda wasicheze karibu na Runners wao(Chasambi na Balua) hii ikafanya Musindo & Chilambo kuacha space kubwa baina yao na Kipre, Iddi Nado & Syllah hali iliyowapa urahisi viungo wa Simba kuzuia uhatari wa Azam kuanzia mstari wa katikati
  2. Azam walikuwa wanaacha spaces kubwa sana baina ya mchezaji mmoja na mwingine + kukosa uharaka kwenye Transition (Ngoma, Kanoute na Mzamiru wakapata machaguo mengi na kukimbia eneo kubwa la uwanja)

Simba kwenye Build-up yao walitumia 2-3-2-3(CBs wawili juu yao Ngoma + Israh & MH15 then Kanoute & Mzamiru mwisho Freddy, Balua na Chasambi)! Simba Leo walipata njia za kupiga pasi kwenda mbele shida ilikuwa kwa L/RWs wao ambao kwenye 1 vs 1 walipata ugumu mbele ya FBs wa Azam FC + Fuentes na Bangala ambao pia walisogea pembeni kuziba makosa ya wenzao

2ND Half! Kila Timu ikaongeza kasi hasa wakivuka mstari wa katikati Simba wakaanza kufanya Quick Transition kupitia katikati huku Azam FC wakati huo ndio wanakosa hicho kitu! Simba wakatumia vizuri nafasi walizopata Dakika 45 za pili kumaliza mchezo wa leo.

THIRD EYE. 📝

  • Juma Mgunda nahisi kama kuna sehemu anafanikiwa sana pale Simba basi ni Dressing Room. I THINK.
  • Mzamiru Yassin wa Mgunda huwa ni mwingine kabisa
  • Balua & Chasambi good players, wanahitaji dakika nyingi tu za kucheza
  • Sadio Kanoute ni mzuri sana akicheza karibu na Box la mpinzani ✅
  • Ayoub Lakred saves & confidence! Chilambo ✅! Msindo what a Fullback
  • Yahya Zaydi ni vile Azam wamepoteza mechi tu! Freddy Koublan kwa sasa kajiamini tayari! Che Malone ✅
  • Mohamed Hussein (MH15) jasho lake Yule Fuentes Mendoza ni mtu sana

NB:Leo Mtani kufurahi Mnyama kushinda

FT: AZAM FC 0-3 SIMBA SC

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz 

7 Comments

  1. Mimi kama mwananchi nimefurahi sana Fei toto na watoto wenzake kuzimwa na kulambishwa Ice cream zao

Leave A Reply


Exit mobile version