Kwenye msimamo wa Ligi Kuu ni tofauti michezo minne kati ya Azam FC na Yanga SC, Azam wanaongoza Ligi wakiwa na jumla na alama 44 huku Yanga SC wakiwa na alama 43. Hapo Yanga ina michezo minne mbele, wapinzani wake pamoja na Simba SC ni kama wameanza kutupa mashuka kwenye huu mpambano na ikitokea wamemfunga Namungo FC unaweza kusema Yanga SC hawana mpinzani kwenye kuutetea Ubingwa wao msimu 2023/2024. Niambie, Chama asifafanishwe na mchezaji yoyote?

Ukiwatazama Simba ni wazi kuwa kuna mambo mengi sana ambayo bila shaka huwezi kuwalaumu wachezaji zaidi sana lazima uwalaumu viongozi na ndio hapo nasema kuwa kutokana na kwamba kuna  maamuzi mengi sana ambayo lawama zote zinaangukia katika uongozi.

Simba iliuchagua uwanja wa Jamhuri Morogoro kama uwanja wake wa nyumbani ila cha kushangaza, wachezaji wa Simba wameenda kwenye mechi dhidi ya Prisons huku wakiwa hawajafanya mazoezi kabisa katika uwanja huo. Timu kubwa itafanyaje kosa kubwa la kiufundi kama hilo?

Baada ya kuwatesa vya kutosha mashabiki wa Dar es Salaam hadi mpaka leo wengi sana wameikatia timu tamaa, sasa uongozi umeamua kuwapelekea uchungu mashabiki wa Simba wa mikoani. Sababu ya kuukimbia Chamazi siyo ishu za kuhujumiwa kama wanavyodai, ni kwa sababu mashabiki wa Dar hawana mwamko sana na hii timu kwa sasa. Bado huko mikoani unaweza kuwaokota okota wakajaza uwanja ila sio kama zamani.

Tukiendelea hivi, na hao wa mikoani nao watakata tamaa na hii timu na baada ya miaka 2 Simba itakuwa timu ya kawaida sana katika ligi. Huwezi kutegemea ubingwa Kama timu yako haina mwendelezo wa kupata matokeo, Leo timu inapata sare kesho inapigwa keshokutwa inashinda!

Timu zinazocheza kibingwa zinapata matokeo hata zikiwa kwenye hali ngumu kudondosha alama ni kitu wanapambana kisitokee kwanza kuchagua uwanja wako wa nyumbani ambao hizi timu za mikoani zinakuwa na advantage kucheza kwenye viwanja Kama vile alafu unataka utoboe.

Mwana kulitaka mwana kulipewa!

SOMA ZAIDI: Simba Waliichukulia Poa Prisons Wameadabishwa

1 Comment

  1. Pingback: Kuondoka Kwa Benchikha Tuitegemee Simba Hii Yenye Matola - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version