Swali langu ni dogo sana kuhusu Azam FC kukosa ubingwa wa Ligi Kuu. Kama tunaitazama Azam FC haina mvuto kwa upande wa KIBIASHARA Sasa hua tunatumiaga vigezo vipi kuwalaumu wanaposhindwa kuchukua ubingwa?

Si hua tunatoka mbele kwenye mike na kuandika sana makala nyingi tukionyesha kuchukizwa ni kwanini Azam na utajiri walionao wanashindwaje kuwa Mabingwa wa Ligi yetu. Leo imetokea anashindana kuisaka nafasi ya pili tayari tunaanza kuzitafuta sababu kuwa, KIBIASHARA hana mvuto.

Jamani siku tutakapoamua kuuweka kando mpira BANDIA, mpira MCHONGO ndio siku hiyo hiyo mpira wetu utapaa zaidi na katika nimegundua kitu, kumbe hata kule kimataifa uwezo wa kuchukua ubingwa tunao sema kuna sehemu hakupo sawa, hili neno wachache sana watanielewa.

Kitu siombei tena sitaki itokee huko mbele isije ikatokea mtindo kama wewe ni shabiki wa Yanga SC basi hupaswi kufanya kazi kituo Fulani cha Radio au kama ni Simba SC ofisi hii huajiriki. Hiki kitu naomba sana kisije kutokea maana tutagawanyika makundi makundi. Leo Tanzania wameibuka watu wachache ambao siyo watu wa mpira kazi yao ni kupotosha umma wazi wazi kisa tu ana Followers wengi na anaaminiwa,

Hii ni hatari sana kwa afya ya mpira wetu. Mtu amekuja kwa kimvuli ni shabiki wa Yanga au Simba, hajui mpira yeye ni mtu mpotoshaji mtu wa chuki Sasa watu wa aina hii tusipowakemea mapema tunakoelekea siyo kuzuri. Mpira umebeba maisha ya watu wengi kwani kitu kinachoweza kubeba hisia ni roho kamili.

Njoo Tujadiliane Zaidi Nipo Kijiweni SHAFFIH DAUDA VS ZAKA ZAKAZI NANI YUKO SAHIHI? 

Njoo Usome Riwaya Za Kijiweni Sasa HADITHI ZA KIJIWENI

Leave A Reply


Exit mobile version