Klabu ya soka ya Azam wameufunga mwaka rasmi kwa kutangaza kufikia makubaliano na klabu ya El Mereikh kwa ajili ya kumsajili kipa wao wa kimataifa wa Sudan, Mohamed Mustafa.

Golikipa huyo amejiunga na klabu ya Azam kwa mkataba wa miezi 6  ambapo atakua katika viunga vya Azam complex kwa mkopo ambapo anatarjiwa kujiunga moja kwa moja kikosi cha kwanza baada ya magolikipa tegemeo wa klabu ya Azam Ali Ahmad ana Iddrisu Abdullai kukabiliwa na majeraha yaliyowapeleka Afrika Kusini kwa matibabu.

Kabla ya kumtambulisha golikipa kikosi cha Azam kimemtambulisha mshambuliaji raia wa Colombia Franklin Navarro ambaye tayari amejiunga na kikosi cha Azam kwenye kombe la mapinduzi Zanzibar.

Endelea kusoma zaidi kuhusu usajili na dondoo mbalimbali kwa kugusa hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version