Ukizungumzia moja kati ya washambuliaji ambao kwa namna moja ama nyingine walikua na msaada mkubwa katika kikosi cha Azam Fc basi huwezi kuacha kutaja jina la mwanamfalme Prince Dube ambaye amekua moja kati ya mpambanaji mkubwa katika kikosi hicho.

Kama mnakumbukumbu wa wakati ule wa sakata la Feisal Salum kushinikiza kuvunja mkataba na Yanga kwenda Azam FC kinyume na utaratibu wengi walisema kuwa hili ambalo wanalolifanya Azam FC na Yusuf Bakhresa wanatengeneza kansa mbaya kwenye soka la Tanzania, haitaishia kwa Yanga tu kama baadhi ya watu wanavyodhani bali itaendelea kutafuna katika vilabu mbalimbali nchini.

Matajiri watatumia sakata la Feisal kama shamba darasa ili kurubuni wachezaji wenye mikataba halali na timu zao wakiwa hawana uoga kwamba sakata litaisha tu kwa busara kama ilivyokuwa kwa Feisal.

Unaweza kudhani labda nimechanganyikiwa au nawachukia matajiri wa Chamazi lakini ukweli ni kwamba nafurahia sana mafanikio yako ambayo wako nayo ila kile ambacho walikianzisha ni wazi kuwa wao walifanikiwa lakini kitawatafuna zaidi pia wao wenyewe na kuwafanya wapate migogoro na wachezaji wao.

Ni wakati wao sasa kujitathmini na kuona wanajiandaaje katika kupambana na changamoto kama hizi ambazo mara nyingi hutokea ile kauli ya busara itumike kumaliza jambo hili kwani kwa asilimia kubwa kabisa ni wazi sakata la Prince Dube kushinikiza kuvunja mkataba na Azam FC linafanana vilevile kama la Feisal Salum Abdallah. Azam wanahaha muda huu, wamesahau kwamba waliwahi kuwa mshirika mkuu wa hili.

SOMA ZAIDI: Timu Zinazoongoza Kwa Udhamini Ligi Kuu Ya Nbc

1 Comment

  1. Pingback: Barua Kwako Mwanamfalme Prince Dube - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version