Mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliowakutanisha klabu ya Azam kutoka Tanzania pamoja na Al Hilal kutoka Sudan umemalizika kwa klabu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1:1.

Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi , ulianza saa 12 jioni huku ikishuhudiwa Al Hilal wakienda mapumziko kifua mbele kwa goli walilofunga kipindi cha kwanza kabla ya Azam kurudi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa Kipre Jr.

Licha ya kuwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulikua na maana kubwa kwa Al Hilal ambao walikua wanajiandaa na mchezo wa makundi klabu bingwa barani Afrika dhidi ya ES SAHEL utakaochezwa tarehe 19 ya mwezi wa 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 4 za usiku.

Azam wao wameendelea na maandalizi yao ya kujiweka sawa na mechi walizonazo mbele yao ikiwemo Ligi kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la shirikisho la Azam.

Unamjua mchezaji bora wa kike wa mwaka barani Afrika na rekodi zake? Msome hapa

Leave A Reply


Exit mobile version