Achilia mbali umbo lake alilonalo na angalia namba ya jezi yake mgongoni kisha soma jina lake vizuri, anaitwa Awesu Awesu, fundi mmoja wa mpira kusema ukweli tu hazungumzwi sana hapa nyumbani lakini  kijana anaujua sana huyu. Katika mechi nyingi ambazo amekua akicheza mtazame kwa umakini kabisa utaelewa kile ambacho ninakuambia hapa.

Nitaukumbuka msimu ule ambao  kiungo huyu alitakiwa na klabu ya Yanga akaona hatatoboa ambapo aliamua kuitupilia  mbali ofa ile na yeye kutimkia kwa matajiri wa Chamazi, Azam FC na baadae kutolewa kwa mkopo KMC FC akitokea hapo Azam, miguu yake inashawishi kiukweli anajua kuwakunisha vichwa maboss huyu ingawa sijui lakini kama ataendelea kubaki alipo sasa.

Anavyocheza katika dimba la kati ni wazi unahitaji kuwa na viungo wenye jicho la mapema kugundua jinsi ya kumzuia kwani anaonesha balaa lake alilonalo na jinsi anavyouonesha uchawi wake katika kukaba na kutoa pasi muhimu wakati wa kushambulia.

Awesu ni miongoni mwa wale wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania wanaotuonesha umuhimu wa kutumia juhudi zao binafsi kama chachu ya kufikia ufanisi. Kujituma kwa kufanya mazoezi kwa bidii, kushiriki kikamilifu katika mechi, na kujitolea kwenye mafunzo kunaweza kuwa njia muhimu ya kuboresha uwezo wao na kufikia viwango vya juu vya mpira wa miguu.

Kwa ujumla mafanikio ya wachezaji wa Ligi Kuu yanaleta heshima kwa taifa kwani wanapofanya vizuri kimataifa au wanapochaguliwa kuwakilisha timu ya taifa, wanachangia katika kujenga taswira chanya ya mpira wa miguu nchini. Hii inaweza kuwahamasisha wachezaji wengine na kuwaleta pamoja Watanzania kusherehekea mafanikio yao.

Kwa kuhitimisha, kujituma kwa wachezaji kama anavyofanya Awesu ni muhimu sana katika kufikia mafanikio makubwa. Ni jukumu letu kama jamii kuwapongeza na kuwatia moyo, kutoa sifa njema wanazostahili, na kujenga mazingira yanayowawezesha kufikia uwezo wao kamili. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kushuhudia maendeleo makubwa katika soka la Tanzania na kufurahia mafanikio ya wachezaji wetu.

SOMA ZAIDI: Guede Amebeba Mzigo Mgumu Usioonekana Kikawaida

 

1 Comment

  1. Pingback: Kiburi Cha Chama Kinalindwa Na Mashabiki Wa Simba - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version