Mwanzo ilionekana kama Asec dhidi ya Simba ni mechi ya kawaida na haitakuwa ngumu kiasi hicho kwa sababu tayari Asec Mimosa ameshafuzu hatua ya Robo fainali lakini si hivyo tena.

Michuano kama hii ambayo huwa inaoneshwa na vyombo vingi vya habari  wachezaji hujituma na kuhakikisha kuwa wanaonesha viwango vyao ili waweze kuonekana na mawakala wakubwa ambao huamini kuwa Afrika kuna vipaji vikubwa sana.

Tunaona namna ambavyo wachezaji wengi wa ASEC MIMOSAS lakini pia hata wa klabu ya Simba ambao kupitia michuano hii wamekua wakipata ofa kutoka klabu nyingi za nje ya nchi ambazo wanachezea soka lao la klabu kwa ujumla.

Ni njia ambayo pia vilabu hutumia kufanya biashara za wachezaji na kuwafaidisha kwa ujumla na kuiongezea klabu mapato ni kama ambavyo Simba ilivyomuuza Chama kabla hajarudi au kama ambavyo Asec hufanya kwa ukubwa sana katika biashara hii kwa bara la Afrika.

Sitegemei kuona wachezaji wa timu zote wakicheza mchezo wa kawaida sana zaidi ya kasi kwa sababu ni mechi muhimu kwa timu zote mbili kwanza Simba anataka kujiwekea nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali lakini pia kwa Asec wao wanataka kumaliza vinara ili wasikutane na vigogo ambao mara nyingi humaliza vinara wa kundi ili wakutane na timu zilishokia nafasi ya pili.

SOMA ZAIDI: Vita Ya Mbinu Itakavyoamua Asec Mimosas vs Simba Sc

1 Comment

  1. Pingback: Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version