Wakiwa nyumbani msimu huu klabu ya Arsenal katika mechi 5 za mwisho wamepoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya West Ham kwa mabao 2:0 huku wakishinda michezo 4 dhidi ya Brighton kwa bao 2:0, Wolves 2:1, Lens 6:0 na Burnley 3:1 na leo wanawakaribisha Liverpool katika uwanja wa Emirates hatua ya 32 bora michuano ya FA.

Liverpool wanaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare dhidi ya Arsenal katika mchezo wa ligi kuu waliocheza katika uwanja wa Anfield kabla ya Krismas huku rekodi ya washika mitutu wa London katika kombe la FA haswa wakiwa nyumbani chini ya Arteta katika michezo 49 wameshinda michezo 36 na kupata sare michezo 10.

Toka mwaka 2018 mechi inayowakutanisha Arsenal dhidi ya Liverpool imekua ya ushindani mkubwa sana huku majogoo wao wakiwa wababe zaidi mbele ya Arsenal kwani wameshamfunga mechi nyingi kati ya zile wanazokutana na  ni mechi moja pekee ambayo iliisha bila kufungana kwani mechi nyingine zote huisha kwa magoli zaidi ya 1.

Arsenal wanaingia katika mchezo huu huku wakiwa wamepoteza mechi 2 mfululizo za mwisho za ligi kuu ambazo ni dhidi ya Fulham kwa bao 2:1 na mechi dhidi ya West Ham kwa bao 2:0 na leo kibarua chao ni dhidi ya Liverpool.

VIDOKEZO VYA UBASHIRI

Katika mchezo huu Liverpool anaingia katika mchezo huu akiwa na asilimiakubwa ya ushindi lakini pia ni wazi kumuheshimu Arsenal hivyo ni bora umpe yoyote ashinde (Home or Away to win 12)

Mechi inayowakutanisha wababe hawa huwa na magoli au kufungana kati yao hivyo ni Both Team to Score and Over 1.5

Msimu huu kumekua na matukio mengi yanayohusisha VAR katika mechi za Arsenal lakini pia za Liverpool unaweza bashiri VAR to be checked kwa wale wenye option hiyo

Endelea kusoma zaidi vidokezo vya ubashiri kwa kugusa hapa.

1 Comment

  1. Pingback: Man City vs Huddersfield: Ubashiri Na Vidokezo Vya Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version