Arsenal wapo karibu kukubaliana na West Ham kuhusu ada ya Declan Rice na inatarajiwa watatoa zaidi ya pauni milioni 100 kwa kiungo huyo ikiwa malipo ya ziada yatapatikana,” linasema gazeti la The Guardian.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, “ombi bado halijawasilishwa lakini mazungumzo kati ya vilabu vinaendelea vizuri na kuna imani kuwa makubaliano yatakamilishwa hivi karibuni.”

The Guardian pia linasema kuwa “Arsenal pia wanazingatia kutoa zabuni kwa kiungo wa Brighton, Moisés Caicedo, ambaye anatafutwa na Chelsea, na wanajaribu kumsaini Ilkay Gundogan wa Manchester City kwa mkataba usio na malipo.”

Per Mertesacker ameiambia kituo cha televisheni cha Ujerumani kuwa anafikiri Arsenal wapo katika “nafasi nzuri” ya kumsaini Ilkay Gundogan kutoka kwa mahasimu wao wa taji la Premier League, Manchester City, kulingana na gazeti la The Mirror.

Soma zaidi hapa kwa taarifa za usajili duniani.

Arsenal pia inaelezwa kuwa inatafuta fursa za kuondoka kwa Nicolas Pepe na Cedric Soares.

Pepe bado ni mchezaji ghali zaidi wa Arsenal tangu alipowasili kwa pauni milioni 72 kutoka Lille mwaka 2019.

Alitumia msimu uliopita kwa mkopo Nice na ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa Arsenal.

Cedric alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo Fulham na pia anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa Arsenal.

Pablo Mari pia anatarajiwa kufanya uhamisho wake wa mkopo kwenda Monza kuwa wa kudumu.

Bayer Leverkusen wana matumaini ya kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo Granit Xhaka.

Kwa kawaida, Arsenal wanataka kuwa na uhakika kuhusu mchezaji mbadala kabla ya kuruhusu uhamisho huo.

Xhaka, mwenye umri wa miaka 30, ana mwaka mmoja uliobaki katika mkataba wake, na chaguo la kuongeza mwaka mmoja.

Mazungumzo kati ya washika mitutu wa London na wawakilishi wa Folarin Balogun yanaendelea kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo.

Kuna nia kubwa kutoka ligi kuu ya Premier na Ulaya kwa Balogun.

Ana miaka miwili iliyobaki katika mkataba wake wa Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga mabao 21 katika ligi kuu akiwa kwa mkopo Reims msimu uliopita na anataka kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.

Leave A Reply


Exit mobile version