Ni miaka 27 pale ambapo mwana mama Adele Onana alipomleta duniani kijana wao ndani ya mji wa Nkol Ngok ndani ya kabila la Yaounde Fang linalopatikana Magharibi mwa Afrika.Francois Onana akiwa na furaha ya kumpata kijana wao wa kiume kati ya Vijana wanne wa familia hiyo aliamua kumlea kijana wao kwenye kijiji cha Nkol Ngol nchini Cameroon akiwa na maisha ya kawaida tu. Andre Onana alizaliwa tarehe 02 ya mwezi wa 4 mwaka 1996 kwenye kijiji cha Nkol Ngok kikiwa karibu na kijiji cha KNkolngok na Ovabang,

Maisha yake ya soka yalianzia nyumbani kwao kwenye ardhi ya Raisi wa Cameroon Paul Biya ndani ya Academy ya mshambuliaji wa zamani na mfungaji bora wa muda wote wa AFCON Samuel Etoo ifahamikayo kama Samuel Etoo’s Academy ambapo alidumu hadi mwaka 2010.

Wakati akiwa na miaka 14, Onana alipata nafasi ya kujiunga na timu ya vijana ya FC Barcelona maarufu kama La Masia ambapo alidumu hadi 2015 na akiwa FC Barcelona msimu wa 2012 hadi 2013 kipa huyo alitolewa kwa mkopo kwenye timu ya Cornella ambayo kwa sasa inashiriki Ligi ya “Primera Federacion” nchini Hispania. Hata hivyo alivyotoka hakurejea moja kwa moja FC Barcelona ila alitolewa tena kwa mkopo kwenda klabu ya Vista Alegre na baada ya kumaliza mkopo wake alirejea FC Barcelona.

Akiwa na miaka 20 Msimu wa 2015 /2016 alisaini mkataba wake wa Soka la kulipwa kwa mara ya kwanza na klabu ya Jong Ajax ya Uholanzi inayoshiriki Ligi ya Eerste Divisie ambapo alidumu kwa msimu mmoja akicheza michezo 39. Msimu wa 2016 aliondoka Jong Ajax na alijiunga na kikosi cha Ajax Amsterdam ya Uholanzi inayoshiriki Ligi ya Eredivisie na hapa ndiyo ukawa mwanzo wake wa kutambulika kwenye ramani ya soka barani Ulaya na duniani.

Ajax Amsterdam ndiyo klabu ambayo alihudumu kwa muda mrefu akicheza kwa miaka saba na akifanikiwa kubeba ubingwa wa Eredivisie mara tatu hadi 2022 alipojiunga na International Milan na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Copa Italia pamoja na SuperCopa Italian huku akishuhudiwa akicheza fainali mara moja ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Haikuwa mwisho safari ya maisha yake ya soka kwa sasa yapo ndani ya Old Traffoed “The theatre of Dream” uwanja wa nyumbani Manchester United akitokea  Inter Milan. Ndani ya Manchester United Andre Onana amekuwa na takwimu bora sana kwani, ameshacheza michezo 21 ya EPL akifanikiwa kupata “Clean Sheet” 6 huku akifanikiwa kufanya Save 72, akiruhusu magoli 29 kadi 3 za njano.

Licha ya kuwa Golikipa lakini Andre Onana amepiga jumla ya pasi 737 mpaka sasa kwenye michezo yote ya EPL aliyocheza. Upande wa Timu ya taifa amefanikiwa kushiriki michuano ya AFCON mara tatu na amecheza jumla ya michezo 12, ambapo 2019 michuano hiyo ilifanyika nchini Misri na alifanikiwa kucheza michezo minne, 2022 ilipofanyika nchini Cameroon alicheza mechi 7 na kupata kadi moja ya njano huku 2024 akicheza Mchezo mmoja tu dhidi ya Senegal.

Pia ameshiriki michezo ya kufuzu Kombe la dunia mara mbili ambayo ni mwaka 2019-2022 na alicheza jumla ya michezo 4 huku 2023-2025 akiwa ameshacheza mchezo mmoja tu.

Moja ya misuko suko aliyowahi kupitia Kipa huyo kupitia ni pamoja na wazazi wake hususa baba yake mzazi Francois Onana alikuwa ataki kijana wake huyo acheze mpira ila alimtaka apambane na shule kwa sababu aliamini kuwa mchezo wa mpira wa miguu unakuweka hatarini muda wowote ule unaweza kupata “Injury” na kushindwa kujua kipi kitaendelea mbeleni hivyo aliamini Shule ni salama zaidi.

Maisha yake ya soka yalisababishwa na kaka yake ambaye alikuwa akicheza Soka na alikuwa Kipa kabla ya kuanza kucheza kama Beki wa kati, kitu kilichomvutia ni pale kaka huyo alipopata ofa Jakarta nchini Indonesia na hapo alivutiwa zaidi kucheza mpira. Upande wa utajiri wake, Inakadiriwa kuwa Andre Onana ana utajiri wa $5M sawa na Bilioni 1.35, huku akiwa amesaini mkataba wa miaka mitano na Man Utd unaokadiriwa kuwa na malipo ya $7M kwa mwaka kama mshahara.

SOMA ZAIDI: Walioleta VAR AFCON wana nafasi yao moyoni mwangu.

Leave A Reply


Exit mobile version