Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Norway ‘Eliteserien’, Amahl Pellegrino anayekipiga Bodo/Glimt ni miongoni mwa wachezaji 53 walioitwa na Kocha Adel Amrouche katika kikosi cha awali cha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Ivory Coast Januari 2024.

Pellegrini (33), aliyezaliwa na kukulia Norway msimu uliopita nyota huyo mwenye asili ya Zanzibar aliekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Norway baada ya kumaliza akiwa na mabao 24 ambayo yaliiwezesha time yeke kuchukua ubingwa wa ligi. Mbali na Pellegrino majina mengine Mapya kwenye kikosi cha awali ni pamoja na Zion (Aldershot Town) na Roberto (Forfar Athletic).

Hatua ya mwisho ya kutaja kikosi cha wachezaji 30 watakao iwakilisha Tanzania kwenye mashindani ya AFCON mwakani inatazamiwa kuwa hivi karibuni na inaelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa safari hii mastaa wanaocheza nnje ya nchi wakapata nafasi kubwa zaidi ya wale wanaocheza Tanzania haswa kwa wale wanaotoka nnje ya timu kubwa tatu.

Endapo itakuwa hivyo, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuhusisha nyota wengi zaidi wanaosakata soka nnje ya ardhi ya Tanzania kuitwa kwenye mashindano. Hata hivyo, jambo hili linafaa kutekelezwa kwa umakini ili kuzuia hali ya sintofahamu ya kujihisi kubaguliwa kwa wachezaji walioitumikia Taifa stars kwenye harakati za kuwania nafasi hii.

Wachezaji wengine waliochaguliwa katika kikosi cha awali cha Tanzania ni hawa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version