Neville alikuwa ameulizwa na Jamie Carragher katika kipindi cha Monday Night Football, iwapo angependelea kuwa na Ronaldo au Weghorst katika kikosi cha sasa cha Man United.
Weghorst aliletwa kwa mkopo kutoka Burnley katika dirisha dogo la uhamisho mwezi Januari, mwezi mmoja baada ya mkataba wa Ronaldo katika Old Trafford kufutwa.
Hata hivyo, Mholanzi huyo amekuwa akikabiliwa na changamoto ya kuonyesha kiwango chake, akifunga mabao mawili tu katika michuano ya kombe. Lakini Neville anaamini kuwa anatoa mchango zaidi kwenye timu kuliko Ronaldo.
“Weghorst ameshinda mechi 12, sare 4, amepoteza 3, amefunga mabao 2 tu lakini timu imefunga mabao 37, wakati Ronaldo alikuwa naanza mechi 19, walishinda mechi tatu chini, sare tatu, walipoteza mechi nne zaidi akiwa kwenye timu, alifunga mabao 11 lakini timu yenyewe ilifunga mabao 23 tu, hii ni tofauti kubwa sana,” alisema Neville.
“Ukweli ni kwamba unaweza kuwa na mchezaji ambaye hafai kuwa mshambuliaji wa Manchester United lakini amekuwa mchezaji mwenye faida zaidi kwa timu. Ninaamini kuwa yeye (Ronaldo) ni mchezaji bora zaidi wa wakati wote.”
Man United ilishuka hadi nafasi ya tano kwenye jedwali la ligi baada ya sare ya 1-1 ya Tottenham na Everton.